Monday 25 September 2017

Kocha Mourinho anusurika na adhabu zaidi

LONDON, England

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho (pichani) hataadhibiwa zaidi baada ya Jumamosi kutolewa uwanjani wakati timu yake ikicheza dhidi ya Southampton.

Mourinho alitolewa nje na mwamuzi Craig Pawson baada ya kuingia uwanjani katika dakika za majeruhi katika mchezo ambao timu yake ilishinda bao 1-0 kwenye Uwanja wa St Mary's.

Baada ya kupokea taarifa ya mwamuzi, Chama cha Soka (FA) kiliamua kutomuongezea adhabu kocha huyo.


Mourinho alifungiwa kuhudhuria mechi mbili na FA msimu uliopita kutokana na matukio tofauti.

No comments:

Post a Comment