Wednesday 13 September 2017

Kocha Mbeya City wa kwanza kutimuliwa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017-18

Na Mwandishi Wetu

KINNAH Phiri (pichani) amekuwa kocha wa kwanza kutupiwa virago msimu huu baada ya kutimuliwa na klabu ya Mbeya City ya Mbeya inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, imeelezwa.

Phiri ambaye ni kocha waamani wa timu ya taifa ya Malawi na klabu ya Free States ya Afrika Kusini, alitupiwa virago baada ya kuitumikia timu hiyo kwa takribani mwaka mmoja.

Katibu wa Mbeya City akizungumza na Azam TV katika kipindi cha Michezo cha Mshikeshike Viwanjani  usiku huu, Emmanuel Kimbe alisema kuwa, kocha huyo ametimulia kufuatia kufanya vibaya kwa timu hiyo msimu uliopita.


 Timu hiyo ambayo ilitamba sana msimu wa mwaka juzi, imeanza vibaya pia katika mechi za msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment