Monday 25 September 2017

Valencia yaipiku Real Madrid katika La Liga

MADRID,Hispania

VALENCIA imewapiku mabingwa watetezi wa La Liga Real Madrid kwa kupanda hadi nafasi ya nne wakati bao la ushindi likifungwa na Simone Zaza dakika tano kabla ya mchezo kumalizika na kushinda 3-2 dhidi ya Real Sociedad jana.

Hatahivyo, kocha wa Valencia Marcelino alijikuta matatan baada ya kujmia misuli wakati akishangilia ushindi wa timu yake.

Marcelino aliumia misuli katika mguu wake wa kushoto wakati akishangilia goli la ushindi la Simone Zaza alilofunga katika dakika ya 85 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Anoeta.

"Nimezeeka, nahitaji kujizuia katika hali fulani, “alisema kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 huku akitabasamu. "Wakati kocha anapoumia, hilo sio tatizo.”

Valencia ilishinda mabao 3-2 na kuendeleza rekodi ya kutofungwa na kupaa hadi katika nafasi ya nne katika msimamo wa La Liga wakati Real Madrid wako katika nafasi ya tano.


Jumla ya mabao 20 yalifungwa katika mechi za La Liga Jumapili wakati Espanyol, Getafe na Celta Vigo nazo pia ziliposhangilia ushindi.

No comments:

Post a Comment