Sunday 24 September 2017

Tigo Fiesta 2017 yafunika kinoma Mwanza

 Ben Pol akifanya vitu vyake kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

NAWEZA  kusema ilikuwa shoo ya aina yake ambayo mikoa mingine ilikopita Tigo Fiesta 2017 mwaka huu haijatokea. Watu waliitikia wito kwa kuujaza Uwanja wa CCM Kirumba na kupata walichotarajia.

Ufunguzi wa jukwaa uliofanya na msanii wa kufokafoka Rosa Ree, ambaye alionesha jinsi gani anakuja kwa kasi kubwa na nyimbo zake zikiwemo mchaga mchaga na up in the air na kufuatiwa na Lulu Diva

 Sehemu ya umati wa wapenzi wa muziki waliofunika CCM Kirumba, Mwanza.

Wasanii Rostam akiwemo Roma na Stamina wao walikuja kivingine walipopanda jukwaani kila moja na baiskeli yake na kuweka kitu tofauti kwenye wimbo wao huku ama kule, kwa kweli ilikuwa burudani tosha.

Wasanii wengine waliofanya shoo iwe na bora kuliko zilizopita ni Ommy Dimpoz na Rayvanny ambao hawakushiriki tamasha zilizopita kila mmoja kwa nafasi yake alikonga nyoyo za masha
biki.

Ali Kiba akifunika.

 Msanii ambaye alifunika wote ni Alli Kiba a.k.a King Kiba kwa kweli aliitendea haki steji mashabiki hawakutaka ashuke kila wakati wanaomba arudie kibao chake 'SEDUCE' huu ni wimbo mpya wa Kiba ambao umetokea kupendwa kila kona alirudia mara tatu kutokana na maombi ya mashabiki.

 Kwa upande wa wadhamini Tigo, Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Edgar Mapande alisema mwaka huu tumeamua kudhaminj ili kusaidia vipaji vya wasanii na kuwaletea wateja wetu burudani, kadhalika kuwapatia vifurishi mara wanunuapo tiketi za Tigo Fiesta . Mteja wetu akinunua tiketi anapata Mbs 100, dakika 100 na sms 100 bure .

Tamasha linaendelea ijumaa ijayo mkoani Tabora kwenye Uwanja wa Ali  Hassan Mwinyi.






No comments:

Post a Comment