Monday 25 September 2017

Mashabiki wa soka wafungwa maisha Misri

CAIRO, Misri

MAHAKAMA ya Misri imewahukumu vifungo vya maisha watu wawili kutokana na vurugu zilizosababisha vifo vya watu kibao kwenye Uwanja wa soka mjini hapa Februari 2015.

Angalau watu 19 walikufa uwanjani baada ya polisi kulipua gesi ya kutoa machozi kwa mashabiki wakati wakijaribu kulazimisha kuingia kwenye Uwanja wa Jeshi la Anga.

Watuhumiwa wengine 12 walifungwa vifungo vya kati ya miaka miwili hadi 10 kwa kuhusu kwao katika dhahama hiyo, ambapo wengine wawili waliachia huru.

Tukio hilo lilitokea kabla ya mchezo kati ya Zamalek na  Enppi.

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza wa ligi kubwa nchini Misri kuruhusiwa mashabiki kuingia uwanjani baada ya mashabiki kuzuiwa kushuhudia mechi kutokana na watu zaidi ya 70 kufa uwanjani huko Port Said mwaka 2012.

Watuhumiwa hao walikuwa wakikabiliwa na makosa ya mauaji, kuleta vurugu, na walikuwa wakishtakiwa kukombana na polisi, na kusababisha vurugu.

Pamoja na wawili kufungwa maisha, watatu walifungwa miaka 10, watano wamefungwa miaka saba, watatu walifugwa jela miaka mitatu kila mmoja na mmoja alifungwa miaka miwili.

Washtakiwa wote walikuwpo mahakamani wakati wa hukumu hiyo na ruksa kukata rufaa.


 

No comments:

Post a Comment