Saturday 30 September 2017

Msomi Chuo Kikuu kuongoza Chaneta, Judith Ilunda amuangusha Mama Mbiro katika Ukatibu Mkuu

Na Mwandishi Wetu
MKUFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Physical Education and Sports Scince, Dk Devotha Marwa ndio mwenyekiti mpya wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) baada ya kumshinda Damian Chonya katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo mjini Dodoma.

Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Halima Bushiri anasema kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chaneta sasa ni Anna Gidalia wakati Katibu Mkuu ni mchezaji wazamani wa timu ya taifa ya netiboli ya Tanzania, Judith Ilunda huku msaidizi wake ni Hilda Mwakatobe.

Ilunda alimshinda makamu mwenyekiti aliyemaliza muda wake katika Chaneta, Zainabu Mbiro ambaye aliamua kuwania ukatibu mkuu badala ya umakamu wa rais.

Nafasi ya Uhazini imebaki wazi baada ya mgombea pekee Grace Khatibu kuata kura chache sana na kuamuriwa uongozi mpya wa Chaneta kuandaa uchaguzi mdogo kwa ajili ya kuziba nafasi hiyo ya uhazini.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni pamoja na Yasinta, Julieth, Kilongozi, Asha, Fortunata na Lwiza.

Uchaguzi huo ulisimamiwa na BMT, ambao waliendesha mchujo jana Ijumaa na kumchuja aliyekuwa mwenyekiti wa Chanea, Annie Kibira na kumtaka kuwa mshauri kutokana na hali yake ya afya kutokuwa nzuri.

No comments:

Post a Comment