Saturday 30 September 2017

Maghembe, Msigwa watembelea banda la TAA Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2017 Iringa

Waziri wa Maliasili na Utalii,  Prof. Jumanne Maghembe (kushoto),aliyefungua rasmi maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini,  akikaribishwa na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa,  Hana Kibopile  kwenye banda la maonesho la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani..
Mhandisi Kedrick Chawe (kulia) akisalimiana na mgeni rasmi wa maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini, Waziri wa Maliasili na utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (mwenye ushungi mweupe) na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Richard Kasesela.



 Mbunge wa Iringa, Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) akizungumza na  Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa  Hana Kibopile alipotembelea banda la maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini  la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
Ofisa Usalama wa Kiwanja cha ndege cha Iringa kilichopo Kata ya Nduli, Miyaga Watanda (kulia) akitoa maelezo mbalimbali kwa wanafunzi wa shule ya Wasichana ya Iringa walipotembelea banda la maoneksho ya Utalii ya Karibu Kusini la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).   

No comments:

Post a Comment