Saturday, 30 September 2017
Msomi Chuo Kikuu kuongoza Chaneta, Judith Ilunda amuangusha Mama Mbiro katika Ukatibu Mkuu
Maghembe, Msigwa watembelea banda la TAA Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2017 Iringa
![]() |
Friday, 29 September 2017
Cecafa yaipa Kenya uenyeji Kombe la Chalenji 2017
NAIROBI, Kenya
BARAZA la Vyama
vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki (Cecafa) limeitangaza Kenya kuwa mwenyeji
wa mashindano ya Chalenji ya wakubwa, ambayo hayajafanyika kwa miaka miwili
sasa.
Kwa mara ya mwisho
mashindano hayo ya Chalenji yalifantyika Ethiopia na Uganda ndio ilitwaa
ubingwa huo.
Katika kikao cha
Kamati ya Utendaji ya Cecafa kilichodanyika Khartoum, Sudan, wajumbe walionesha
msiokamano na Kenya dhidi ya kupokonywa uenyeji wa mashindano ya Mataifa ya
Afrika kwa wachezaji wa ndani, Chan Januari 2018.
Mashindano ya wakubwa ya Chalenji yanashirikisha mataifa
yote 13 wanachama wan chi za Afrika Mashariki na Kati, yatafanyika Novemba na
Desemba mwaka huu.
Uganda ndio
mabingwa wasasa wa mashindano hayo baada ya kutwaa kwa ara ya mwisho mwaka 2015
baada ya kuifunga Rwanda 1-0 katika fainali.
Mkutano huo pia
ulizitangaa Burundi na Rwanda kuwa wenyeji wa mashindano ya Cecafa ya vijana
wenye umri chini ya miaka 17 na yale ya wanawake Novemba na Desemba.
Thursday, 28 September 2017
Maghembe Kufungua Maonesho ya Utalii Karibu Kusini yanayofanyika Kihesa mkoani Iringa
Na Mwandishi Wetu,Iringa
Maonesho hayo yenye kaulimbiu ya Utalii
Endelevu ni Nguzo ya Uchumi wa Viwanda yanashirika taasisi za serikali,
mashirika ya umma na kimataifa zaidi ya 400, ambapo yatamalizika Oktoba 2,
2017, ambapo yanalengo la kuweka uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa utalii na
thamani thamani ikiwa ni pamoja na kuutangaza utalii kwa kuihamasisha jamii
kutumia fursa za utalii zilizopo katika kuinua uchumi wa wakazi wa Ukanda wa
Kusini mwa Tanzania na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wa Wizara mbalimbali zipo na
taasisi zake ikiwemo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Idara ya
Utalii, Wanyamapori, Mambo ya Kale na Misitu na Nyuki, Chuo cha Taifa cha
Utalii, Makumbusho ya Taifa, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro, Mamlaka ya Usimamizi ya Wanyamapori (TAWA) Mfuko wa
Misitu Tanzania (TaFF).
Taasisi nyingine ni Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania, (TFS) Taasisi ya
Utafiti wa Misitu na Wadau wa Wizara ya Maliasili na Utalii.Wadau wa Sekta ya
Utalii kutoka mikoa ya Nyanda za Juu
Kusini watashiriki kuonesha bidhaa na huduma zao muhimu na mikoa inayoshiriki
ni pamoja na wenyeji Iringa, Mbeya, Ruvuma, Songwe na Njombe.
Fursa zilizopo nyanda za Juu Kusini ni
pamoja na Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa,
Ismila,Kalenga na Boma la Mkuu wa Wilaya, Hifadhi za Mahale, Katavi,
Ruaha, Kitulo na Selous.Monday, 25 September 2017
LONDON, England
TIMU ya Brighton imeichapa Newcastle United bao 1-0 na kupata ushindi wa pili mfululizo katika mechi za Ligi Kuu ya England.
Wenyeji walipata bao wakati krosi ya Pascal Gross iliporejeshwa nyuma kwa kichwa na Dale Stephens na Tomer Hemed alifunga kutoka umbali wa meta sita.
Newcastle, ambayo ilishinda mechi zake tatu zilizopita, ilikuwa na nafasi, lakini mpira wa Mikel Merino ulipanguliwa na Mat Ryan, huku Joselu mara mbili akishindwa kufunga na mchezaji aliyetokea benchi Jonjo Shelvey, shuti lake likigonga mwamba.
Ushindi huo umeiwezesha Seagulls kupaa hadi nafasi ya 13 katika msimamo, wakati Newcastle imeporomoka hadi nafasi ya tisa.
Newcastle ilitawala zaidi mchezo huo na kupiga mashuti mengi lakini kikosi hicho kinachofundishwa na Rafael Benitez, kilishindwa kulazimisha sare.
Wachezaji waliongia wakitokea benchi Jesus Gamez na Dwight Gayle jitihada zao za dakika za mwisho zilishindwa kuzaa matunda, ambapo mashuti yao yaliokolewa na Ryan.
Wagombea Chaneta kupiga kampeni kiduchu
![]() |
Annie Kibira |
Na Mwandishi Wetu
WAGOMBEA
watakaopitishwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa
Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) Jumamosi mjini Dodoma, watakuwa na muda
mfupi wa kujinadi.
Kwa mujibu wa
ratiba ya uchaguzi huo iliyotolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), mwisho
wa kuchukua na kurudisha fomu ni Alhamisi wakati usaili utafanyika Ijumaa na
uchaguzi Jumamosi.
Mwenyekiti wa
Chaneta, Annie Kibira amesema leo kuwa muda wa kampeni ni mdogo sana, lakini
itabidi kufuata utaratibu uliowekwa na BMT, ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi
huo.
Alisema
hawaruhusiwi kufanya kampeni hadi baada ya usaili kwani kutofuata utaratibu
huo, unaweza kukatwa kwani utakuwa umekiuka utaratibu.
![]() |
Halima Bushiri;Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT). |
Naye Ofisa Michezo
wa BMT, Halima Bushiriki amesema leo kuwa wamepanga ratiba hiyo ili
kuwaepuesha wagombea na wapiga kura kuingia gharama.
Alisema hadi jana wagombea 14 wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali walirudisha fomu kati ya 25 waliochukua fomu hizo, huku akiwasisitizia watu kuendelea kuchukua na kurudisha kwa wakati ili kufanikisha zoezi hilo.
Pia aliwataka wadau mbalimbali wa michezo bila kujali jinsi, yaani wanawake na wanaume wenye sifa kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu hizo ili kugombea uongozi.
Aliwataja waliorudisha hadi jana kuwa ni Annie Kibira (uenyekiti), Dk Devota Muro, Luiza Jellah (ujumbe), Mwajuma Kisengo (katibu msaidizi/mjumbe), Asha Sapi (ujumbe) na Winfrida Emmanuel (makamu mwenyekiti),
Wengine
waliorejesha fomu ni Hilda Mwakatobe (katibu msaidizi), Judith Ilunda (katibu
mkuu/ujumbe), Zakia Kondo (ujumbe), Julieth Mndeme (ujumbe), Pili Mongella
(makamu mwenyekiti/ujumbe).
Kocha Mourinho anusurika na adhabu zaidi
LONDON, England
KOCHA wa
Manchester United, Jose Mourinho (pichani) hataadhibiwa zaidi baada ya Jumamosi kutolewa
uwanjani wakati timu yake ikicheza dhidi ya Southampton.
Mourinho alitolewa
nje na mwamuzi Craig Pawson baada ya kuingia uwanjani katika dakika za majeruhi
katika mchezo ambao timu yake ilishinda bao 1-0 kwenye Uwanja wa St Mary's.
Baada ya kupokea
taarifa ya mwamuzi, Chama cha Soka (FA) kiliamua kutomuongezea adhabu kocha
huyo.
Mourinho alifungiwa
kuhudhuria mechi mbili na FA msimu uliopita kutokana na matukio tofauti.
Valencia yaipiku Real Madrid katika La Liga
MADRID,Hispania
VALENCIA imewapiku
mabingwa watetezi wa La Liga Real Madrid kwa kupanda hadi nafasi ya nne wakati
bao la ushindi likifungwa na Simone Zaza dakika tano kabla ya mchezo kumalizika
na kushinda 3-2 dhidi ya Real Sociedad jana.
Hatahivyo, kocha
wa Valencia Marcelino alijikuta matatan baada ya kujmia misuli wakati
akishangilia ushindi wa timu yake.
Marcelino aliumia
misuli katika mguu wake wa kushoto wakati akishangilia goli la ushindi la
Simone Zaza alilofunga katika dakika ya 85 katika mchezo uliofanyika kwenye
Uwanja wa Anoeta.
"Nimezeeka,
nahitaji kujizuia katika hali fulani, “alisema kocha huyo mwenye umri wa miaka
52 huku akitabasamu. "Wakati kocha anapoumia, hilo sio tatizo.”
Valencia ilishinda
mabao 3-2 na kuendeleza rekodi ya kutofungwa na kupaa hadi katika nafasi ya nne
katika msimamo wa La Liga wakati Real Madrid wako katika nafasi ya tano.
Jumla ya mabao 20
yalifungwa katika mechi za La Liga Jumapili wakati Espanyol, Getafe na Celta
Vigo nazo pia ziliposhangilia ushindi.
Mashabiki wa soka wafungwa maisha Misri
CAIRO, Misri
MAHAKAMA ya Misri
imewahukumu vifungo vya maisha watu wawili kutokana na vurugu zilizosababisha
vifo vya watu kibao kwenye Uwanja wa soka mjini hapa Februari 2015.
Angalau watu 19
walikufa uwanjani baada ya polisi kulipua gesi ya kutoa machozi kwa mashabiki
wakati wakijaribu kulazimisha kuingia kwenye Uwanja wa Jeshi la Anga.
Watuhumiwa wengine
12 walifungwa vifungo vya kati ya miaka miwili hadi 10 kwa kuhusu kwao katika
dhahama hiyo, ambapo wengine wawili waliachia huru.
Tukio hilo
lilitokea kabla ya mchezo kati ya Zamalek na
Enppi.
Mchezo huo ulikuwa
wa kwanza wa ligi kubwa nchini Misri kuruhusiwa mashabiki kuingia uwanjani
baada ya mashabiki kuzuiwa kushuhudia mechi kutokana na watu zaidi ya 70 kufa
uwanjani huko Port Said mwaka 2012.
Watuhumiwa hao
walikuwa wakikabiliwa na makosa ya mauaji, kuleta vurugu, na walikuwa
wakishtakiwa kukombana na polisi, na kusababisha vurugu.
Pamoja na wawili
kufungwa maisha, watatu walifungwa miaka 10, watano wamefungwa miaka saba,
watatu walifugwa jela miaka mitatu kila mmoja na mmoja alifungwa miaka miwili.
Washtakiwa wote
walikuwpo mahakamani wakati wa hukumu hiyo na ruksa kukata rufaa.
Brighton yaichapa Newcastle United bao 1-0
LONDON, England
TIMU ya Brighton
imeichapa Newcastle United bao 1-0 na kupata ushindi wa pili mfululizo katika
mechi za Ligi Kuu ya England.
Wenyeji walipata
bao wakati krosi ya Pascal Gross iliporejeshwa nyuma kwa kichwa na Dale
Stephens na Tomer Hemed alifunga kutoka umbali wa meta sita.
Newcastle, ambayo
ilishinda mechi zake tatu zilizopita, ilikuwa na nafasi, lakini mpira wa Mikel
Merino ulipanguliwa na Mat Ryan, huku Joselu mara mbili akishindwa kufunga na
mchezaji aliyetokea benchi Jonjo Shelvey, shuti lake likigonga mwamba.
Ushindi huo
umeiwezesha Seagulls kupaa hadi nafasi ya 13 katika msimamo, wakati Newcastle
imeporomoka hadi nafasi ya tisa.
Newcastle
ilitawala zaidi mchezo huo na kupiga mashuti mengi lakini kikosi hicho
kinachofundishwa na Rafael Benitez, kilishindwa kulazimisha sare.
Wachezaji
waliongia wakitokea benchi Jesus Gamez na Dwight Gayle jitihada zao za dakika
za mwisho zilishindwa kuzaa matunda, ambapo mashuti yao yaliokolewa na Ryan.
Sunday, 24 September 2017
Tigo Fiesta 2017 yafunika kinoma Mwanza
Ben Pol akifanya vitu vyake kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. |
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
NAWEZA kusema
ilikuwa shoo ya aina yake ambayo mikoa mingine ilikopita Tigo Fiesta 2017 mwaka huu
haijatokea. Watu waliitikia wito kwa kuujaza Uwanja wa CCM Kirumba na kupata
walichotarajia.
Ufunguzi wa jukwaa uliofanya na msanii wa kufokafoka Rosa Ree, ambaye alionesha jinsi gani anakuja kwa kasi kubwa na nyimbo zake zikiwemo mchaga mchaga na up in the air na kufuatiwa na Lulu Diva
Sehemu ya umati wa wapenzi wa muziki waliofunika CCM Kirumba, Mwanza. |
Wasanii Rostam
akiwemo Roma na Stamina wao walikuja kivingine walipopanda jukwaani kila moja
na baiskeli yake na kuweka kitu tofauti kwenye wimbo wao huku ama kule, kwa
kweli ilikuwa burudani tosha.
Wasanii wengine
waliofanya shoo iwe na bora kuliko zilizopita ni Ommy Dimpoz na Rayvanny ambao
hawakushiriki tamasha zilizopita kila mmoja kwa nafasi yake alikonga nyoyo za
masha
biki.
Ali Kiba akifunika. |
Msanii ambaye alifunika wote ni Alli Kiba a.k.a King Kiba kwa kweli aliitendea haki steji mashabiki hawakutaka ashuke kila wakati wanaomba arudie kibao chake 'SEDUCE' huu ni wimbo mpya wa Kiba ambao umetokea kupendwa kila kona alirudia mara tatu kutokana na maombi ya mashabiki.
Kwa upande wa wadhamini Tigo, Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Edgar Mapande alisema mwaka huu tumeamua kudhaminj ili kusaidia vipaji vya wasanii na kuwaletea wateja wetu burudani, kadhalika kuwapatia vifurishi mara wanunuapo tiketi za Tigo Fiesta . Mteja wetu akinunua tiketi anapata Mbs 100, dakika 100 na sms 100 bure .
Tamasha
linaendelea ijumaa ijayo mkoani Tabora kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Tuesday, 19 September 2017
Tetemeko la Ardhi laua Watu 140 nchini Mexico
MEXICO CITY,
Mexico
TETEMEKO kubwa la
ardhi limeikumba Mexico na kupoteza maisha ya zaidi ya watu 140 na kuharibu
majengo mengi katika jiji hili, imeelezwa.
Angalau watoto 21 wanahofiwa
kufa na wengine wakiripotiwa kupotea baada ya shule kuanguka katika jiji hilo.
Tetemeko hilo
linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa magnitude 7.1 pia limesababisha uharibifu
mkubwa katika nchi za jirani.
Kwa mara ya mwisho
tetemeko kubwa kama hilo liliwahi kutokea takribani miaka 32 iliyopita baada ya
tetemeko kuua maelfu ya watu Mexico City.
Hilo ni tetemeko
la pili kutokea baada ya lile la mapema mwezi huu ambalo lilikuwa na ukubwa na
magnitude 8.1 ambalo liliua watu 90 lilitokea kusini mwa nchi hii.
Angalau watu 149
wamekufa nchi nzima, kimeeleza chanzo kimoja cha habari.
Angalau watu 55
wamekufa katika Jimbo la Morelose,kusini mwa Mexico City, huku 32 wakifa huko Pueblae.
Watu 49 wanahofiwa kupoteza maisha Mexico City, huku wengine 10 wakifa katika
Jimbo la Mexico, na watau wakifa huko Guerrero.
Karibu watu
milioni 2 wakazi wa Mexico City wameachwa bila ya umeme huku nyaya za simu
zikiwa zimeanguka. Wananchi wameonywa kutovuta sigara mitaani kwani gesi
inaweza kulipuka.
Meya wa Mexico
City Miguel Angel Mancera aliaimbia TV moja kuwa huduma za uokoaji zinaendelea
kuchimba katika makazi 44 ili kuona kama kuna watu wamefukiwa na kifusi.
Kaimu Katibu wa
Elimu Javier Treviño, alikaririwa na vyombo vya habari vya haba kuwa, watoto 21
na watu wazima wanne walikufa wakati shule ya Enrique Rebsamen iliyopo kusini
mwa Mexico City ilipoanguka.
Baadhi ya
wanafunzi waliokolewa, vyombo vya habari vya Mexico viliripoti, lakini wengine
bado hawajapatikana.
Nyumba za gholofa,
maduka makubwa na kiwanda navyo pia ni baadhi ya vitu vilivyoanguka jijini
hapa.
Akihutubia kupia
televisheni, Rais wa Mexico Peña Nieto alisema dharura imechukulia katika
maeneo yaliyoathirika na jeshi limekwenda kutoa msaada.
Karibu sehemu zote
katika jiji la Mexico, timu ya watu wa uokoaji na wake wakujitolea wamekuwa
wakifanya jitihada mbalimbali kuwaokoa watu.
"Mke wangu
yuko pale. Sijaweza kuwasiliana naye, “alisema Juan Jesus Garcia, 33, huku
akitokwa na machozi jirani na jengo lililoanguka.
"Hajaweza
kujibu simu na sasa tumeambia kuzima simu zetu za viganjani kwa sababu kuna
gesi inayovuja inaweza kulipuka.”
Tetemeko hilo la ardhi
limetokea jijini Mexico wakati wa
kumbukumbu ya miaka 32 ya tetemeko jingine la ardhi lililoua watu 10,000.
Mexico City ni
moja ya majiji yenye watu wengi duniani, ambapo ina zaidi ya wakazi milioni 20
wanaoshi hapo.
Messi atupia manne Barca ikishinda 6-1
BARCELONA,
Hispania
LIONEL Messi ameongeza
mabao manne katika akaunti yake aliyofunga mapema msimu huu wakati Barcelona ikiendeleza
kwa asilimia 100 rekodi yake ya ushindi katika Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga
baada ya kuifunga Eibar 6-1 jana.
Paulinho na Denis
Suarez nao pia walizifumania nyavu katia mchezo wa pili mfululizo wakati Barca ikizidi
kujitanua kileleni katika ,simamo wa ligi hiyo hadi kufikia pointi saba zaidi
dhidi ya wapinzani wao wakubwa, Real Madrid, ambayo leo watakuwa wenyeji wa Real
Betis.
Mapema, Valencia ilipanda
hadi katika nafasi ya tatu wakati Simone Zaza alipofunga mabao matatu `hat-tric’
ndani ya dakika saba wakati timu hiyo ikiisambaratisha Malaga kwa mabao 5-0.
Kocha wa Barca Ernesto
Valverde alikibalisha sana kikosi chake kwa mara ya kwanza tanbgu alipoanza
kuifundisha timu hiyo, ambapo alibadili wachezaji sita kutoka katika kikosi
kilichocheza Jumamosi na kushinda 2-1 dhidi ya Getafe.
Messi alianza
kufungua akaunti ya mabao katika mchezo huo baada ya kufunga kwa penalti katika
dakika ya 21 baada ya Nelson Semedo kuchezewa vibaya na Alejandro Galvez.
Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | Barcelona | 5 | 5 | 0 | 0 | 17 | 2 | 15 | 15 |
2 | Sevilla | 4 | 3 | 1 | 0 | 6 | 1 | 5 | 10 |
3 | Valencia | 5 | 2 | 3 | 0 | 9 | 3 | 6 | 9 |
4 | Real Sociedad | 4 | 3 | 0 | 1 | 11 | 7 | 4 | 9 |
5 | Real Madrid | 4 | 2 | 2 | 0 | 9 | 4 | 5 | 8 |
6 | Atlético Madrid | 4 | 2 | 2 | 0 | 8 | 3 | 5 | 8 |
7 | Athletic Club | 4 | 2 | 1 | 1 | 3 | 1 | 2 | 7 |
8 | Villarreal | 4 | 2 | 0 | 2 | 6 | 5 | 1 | 6 |
9 | Levante | 4 | 1 | 3 | 0 | 5 | 4 | 1 | 6 |
10 | Leganés | 4 | 2 | 0 | 2 | 3 | 3 | 0 | 6 |
11 | Las Palmas | 4 | 2 | 0 | 2 | 5 | 7 | -2 | 6 |
12 | Real Betis | 4 | 2 | 0 | 2 | 5 | 7 | -2 | 6 |
13 | Eibar | 5 | 2 | 0 | 3 | 3 | 10 | -7 | 6 |
14 | Getafe | 4 | 1 | 1 | 2 | 3 | 4 | -1 | 4 |
15 | Girona | 4 | 1 | 1 | 2 | 3 | 5 | -2 | 4 |
16 | Espanyol | 4 | 1 | 1 | 2 | 3 | 8 | -5 | 4 |
17 | Celta de Vigo | 4 | 1 | 0 | 3 | 5 | 7 | -2 | 3 |
18 | Deportivo La Coruña | 4 | 0 | 1 | 3 | 5 | 11 | -6 | 1 |
19 | Deportivo Alavés | 4 | 0 | 0 | 4 | 0 | 7 | -7 | 0 |
20 | Málaga | 5 | 0 | 0 | 5 | 1 | 11 | -10 | 0 |