Monday, 23 January 2017

Uchaguzi Mkuu Chama cha Mpira wa Meza kufanyika Uwanja wa Taifa Februari 11

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Najaha Bakari akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Mpira wa Meza Tanzania (TTA).
Na Mwandishi Wetu
UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Mpira wa Meza Tanzania (TTA), unatarajia kufanyika Februari 11 mwaka huu, imeelezwa.

Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Tanzania (BMT), Najaha Bakari akizungumza leo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa BMT alisema kuwa, fomu kwa wale wanaotaka kuwania uongozi zilianza kutolewa jana Januari 23, ambapo mwisho wa kuchukua na kurudisha ni Februari 6.

Kwa mujibu wa Najaha, usaili utafanyika Februari 9 katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambako uchaguzi huo utakapofanyikia pia.

Nafasi zinazowaniwa ni pamoja na Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu, Katibu Mkuu Msaidizi na Mhazini wakati fomu kwa wanaotaka kuwania nafasi hizo zitatolea kwa Sh. 100,000 wakati wajumbe sita wa kuchaguliwa kila fomu kwao itakuwa ni Sh. 50,000 tu.

Sifa za viongozi kulingana na Katiba ya Chama cha Tenisi Tanzania ni kama ifuatavyo.
1, Awe raia wa Tanzania.
2.Kiwango cha chini cha elimu ni kidato cha nne na kwa nafasi za juu za uongozi.
3.Awe na uelewa na uzoefu katika mchezo wa tenisi
4.Awe na ufahamu wa kutumia komputa
5.Awe na uwezo wa kuongea na kuandika vizuri kiingereza na Kiswahili.

NB
Baraza linatoa wito kwa wenye sifa na wapenda maendeleo ya mchezo huu na maendeleo ya michezo nchini kujitokeza kuchukua fomu kwa wakati ili kufanikisha uchaguzi huo.


Fomu za kugombewa zitalipiwa akaunti ya BMT kwa jina la National Sports Council AC. No. 20401100013 na kuwasilishwa baraza pamoja na risiti iliyolipiwa benki.

No comments:

Post a Comment