Sunday 22 January 2017


Ni kifo Morocco, Ivory Coast

LIBRAVILLE, Gabon


KOCHA wa timu ya taifaya Morocco Herve Renard amebainisha kuwa watapambana kufa au kupona wakati watakapokutana na timu yake yazamani ya Ivory Coast kesho katika mchezo wa Afcon.

Miaka miwili baada ya kuiongoza Ivory Coast kutwaa taji hilo, Renard itakabiliana nao katika robo fainali ya michuano hiyo.
"Najaribu kusahau, kwasababu nilipowaiona Waivory coast kabla ya kufuzu kwa Kombe la Dunia miezi miwili iliyopita, ilikuwa ni hisia kali kwangu, alisema.
"Ilitubidi kupambana na kucheza ili kushindatulitakiwa kuwa na nguvu.

Renard ambaye ni kocha wa Morocco iliifunga Togo 3-1 katika mchezo wa Kundi c Ijumaa na kujiweka katika mazingira mazuri, ikifuatiwa na sare ya Ivory Coast na Congo (DR) ya bao 2-2 katika mchezo wa mapema siku hiyo.

Congo (DR) ndio wanaoongoza kundi hilo wakiwa na pointi nne, Ivory Coast mbili wakati Togo ikiwa na pointi moja.
Ushindi dhidi ya Ivory Coast katika mchezo utakaofanyika Oyem utaiwezesha Morocco kufuzu kwa hatua ya nane bora, lakini hadi sasa timu zote nne katika kundi hilo zina nafasi ya kufuzu.

Morocco ilijiweka katika hatari mjini Gabon, baada ya kufungwa mchezo wa kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya Congo na kuwa nyuma ya Togo Ijumaa kabla ya kubadili matokeo na kushinda 3-1.


Renard aliwapongeza wachezaji wake baada ya kupambana hadi kupata matokeo ambayo yameiweka pazuri timu hiyo.

No comments:

Post a Comment