Sunday 22 January 2017

Kocha Mali awajibika kwa kipigo

KOCHA wa Mali Alain Giresse amesema kuwa kwa timu yake 1-0 na Ghana katika mchezo wa Kundi D katika mashindano ya Afcon yanayoendelea ni kosa lake.
Mfaransa huyo alisema kuwa angeweza kufanya vizuri zaidi katika uteuzi wa timu dhidi ya Black Stars ambao sasa wamefuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.

Nawajibika kwa kipigo hicho dhidi ya Ghana. Ningeweza kufanya vizuri zaidi kwa kutumia wachezaji wa akiba hivyo hakuna ubishi hilo ni kosa langu, “alisema Giresse ambaye kikosi chake kina pointi moja tu baada ya mechi mbili na kikosi katika nafasi ya tatu.

Chipukizi Yves Bissouma, Moussa Doumbia na Kalifa Coulibaly, walioanzia katika benchi, waliingizwa katika kipindi cha pili na kuonesha kiwango kizuri.

Mbinu binafsi za Bissouma na Doumbia ziliishangaza Ghana baada ya majaribio kadhaa ya kipa Razak Brimah,na kama wangeanzia kipindi cha kwanza wangeweza kupata bao.
 Sio tatizo la kujiamini ila ni uzoefu tu. Ilikuwa rahisi kwao kuja na jua kuwa wanaweza kucheza vizuri kwa sababu ilikuwa hatari. Ni vizuri kama wangeingizwa mapema na bila shaka wangefanya vizuri, “alisema
Giresse.


Mali itakabiliana na Uganda katika mchezo mwisho wa Kundi D utakaofanyika Stade dOyem keshokutwa, ambapo timu zote bado hazijafunga wala kushinda katika Afcon 2017.

No comments:

Post a Comment