Friday 20 January 2017

Serikali, DStv wampongeza Simbu kwa kushinda Mumbai Marathon 2017

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili kushoto) akipokea tuzo ya mshindi wa Mumbai Marathon 2017 kutoka kwa mshindi wa mbio hizo, Alphonce Simbu wakati wa hafla ya kumpongez mwanariadha huyo iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania, Wilhem Gidabuday na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania, Shelukindo.
Na Mwandishi Wetu
MSHINDI wa mbio za Mumbai Marathon, Alphonce Simbi amesema kuwa ili Tanzania ifanye vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa, lazima wajiandae vizuri na kushirikisha wanariadha wengi.

Sambu aliyasema hay oleo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla maalum ya kumpongeza iliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice jijini Dar es Salaam, ambayo pia ilihudhuria na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye aliyekuwa mgeni rasmi.

Alisema kuwa kujiandaa vizuri na idadi kubwa ya wanariadha wanaotoka nchi moja katika shindano husika kunasaidia kufanya vizuri kama wanavyofanya Kenya.

Simbu aliwashukuru sana DStv kwa kumdhanini kwani kumesaidia kufanikisha kutimiza ndoto yake ya kufanya vizuri katika mashindano makubwa ya kimataifa.

Alisema Wakenya wamekuwa wakipeleka wanariadha wengi katika mashindano na kwa mfano katika mbio hizo za Mumbai Marathon ilikuwa na zaidi ya wakimbiaji saba, ambao walisaidia sana katika mbio.

Alisema kuwa alimuacha Mkenya katika kilometa 41, ambapo chomoka na kumaliza wa kwanza katika mbio hizo, ukiwa ni ushindi wake wa kwanza katika mbio za marathon.

Simbu aliwashukuru DStv, Riadha Tanzania, mwajiri wake ambaye ni Jeshi la Kujenga Taifa, Waandishi wa Habari na wadau wengine wote wa michezo kwa ushirikiana wao uliomuwezesha kufanya vizuri.

Pia aliomba watu wengine wajitokeze kuwasaidia wanariadha kwa njia mbalimbi ikiwemo kuwapatia maji au mafuta ya magari au pikipiki na vitu vingine ili kuwawezesha kufanya vizuri katika mashindano tofauti tofauti.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice, Shelukindo alimpongeza Simbu kwa ushindi huo wa Mumbai Marathon, ambapo alisisitiza kuwa wataendelea kumsaidia mwanariadha huyo.

Alisema kuwa waliamua kumsaidia Simbu baada ya kushika nafasi ya tano katika Michezo ya Olimpiki ya Rio 2016 ili aweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano mengine makubwa licha ya baadhi ya watu kutotuelewa kwanini tunamsaidia mtu aliyeshika nafasi ya tano.

Alisema kuwa Multichoice itaendelea kumsaidia Simbu, ambapo watajitahidi kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wanachangia sekta zote za michezo na burudani.

Aliwataka waadishi wa habari kuendelea kuandika mema ya nchi yetu.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema kuwa baada ya Simbu kufanya vizuri alihisi kuwa sasa ututukufu wa Tanzania katka riadha umerudi.

Pia aliwapongeza DStv kwa kuwa wazalendo wa kweli katika kuhakikisha michezo inasonga mbele hapa nchini.
Alisema mafanikio ya Simbu ni mfano hai kuwa watu wakiwekeza vizuri mafanikio yataonekana, ambapo aliwapongeza Multchoice kwa msaada wao kwa Simbu.

Alitoa wito kwa wadau wengine wa michezo kujitokeza kuwasaidia wachezaji mbalimbali hapa nchini ili waweze kufanya vizuri.
Alisema watu wa utalii wakiwekeza kutumia wizaya ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kujitangaza badala ya kutumia fedha nyingi kwa matangazo.

Pia aliipongeza JKT kwa jitihada zao za kuvichukua vipaji na kuviendeleza, ambapo alimtaka mwakilishi wa jeshi hilo katika hafla hiyo kumpelekea salamu Mkuu wa Majeshi kwani jeshi lake liko mstari wa mbele kuendeleza michezo nchini.
 

No comments:

Post a Comment