Sunday 15 January 2017

Media Day 2017 ya Multchoice yafana Shekinah Garden, waandishi wa habari washuhudia Diamond akipamba uzinduzi wa Afcon Gabon




Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice-Tanzania, Maharage Chande akisakata dansi wakati wa Bonanza la Waandishi wa Habari lililoandaliwa na Multchoice jana Shekinah Garden Mbezi Beach, Makonde jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Multchoice-Tanzania kupitia king’amuzi chake cha DStv, jana iliwaandalia waandishi wa habari Bonanza la aina yake katika ukumbi wa Shekinah Garden uliopo Mbezi Beachi, Makonde jijini Dar es Salaam.

Katika bonanza hilo ambalo waandishi wa habari walicheza muziki, kupata viwanywaji vya aina mbalimbali na mlo mzito, pia walishuhudia ufunguzi wa mashindano ya 31 ya Mataifa ya Afrika yaliyoanza jana nchini Gabon, huku uzinduzi huo ukipambwa na nyota wa muziki nchini Tanzania, Nassib Abdul au Diamond na kibao chake cha Nana.


Kiongozi wa Kitengo cha Mahusiano cha Multchoice-Tanzania, Johnson Mshana akikonga nyoyo za waandishi wa habari na wageni waalikwa waliofika katika tamasha hilo jana.
Multchoice- Tanzania iliandaa bonanza hilo maalum kwa ajili ya waandishi wa habari katika kuukaribisha mwaka 2017, sambamba na kuwashukuru waandishi wa habari kwa ajili ya ushirikiano wao mzuri katika kipindi kilichopita.


Waandishi wa habari wakisubiri kupata menu wakati wa bonanza hilo la aina yake lililofanyika jana.
Katika mchezo wa ufunguzi uliozikutanisha Burkina Faso na Cameroon, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 huku bao la Burkina Faso likifungwa na Issoufou Dayo wakati lile la Cameroon likipachikwa na Benjamin Moukandjo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice Tanzania, Maharage Chande aliwashukuru waandishi wa habari kwa ushirikiano nao na alisema wataendelea kuwa bega kwa bega katika mwaka huu.

Alisema waandishi wa habari wamekuwa wakitoa mchango mkubwa kuhakikisha DStv inafanya vizuri katika kufanikisha lengo lake la kuonesha michezo kwa uhakika.

Katika bonanza hilo la waandishi wa habari mbali na burudani zingine, kulikuwapo na kundi la muziki wa dansi la La Mwiduka, ambalo lilikonga nyoyo za waandishi na wageni wengine kwa vibao vyao vya kabila la Kisafwa kutoka mkoani Mbeya na lile la Sana Afrika.
Akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari wakati hafla hiyo, mmiliki wa blogo ya Full Shangwe, John Bukuku aliipongeza DStv kwa kuandaa bonanza hilo kwa waandishi wa habari, ambalo alisema litazidi kuimarisha mshikamano uliopo kati ya waandishi wa DStv.










 

No comments:

Post a Comment