Wednesday, 25 January 2017

JKT QUEENS YAIDHIBU MBURAHATI QUEENSNa mwandishi wetu

Ligi ya wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliendelea leo  kwa mchezo kati ya JKT Queens na Mburahati Queens zote za Dar es Salaam zilizo kundi A ,ambapo katika mchezo huo JKT Queens iliifunga Mburahati Queens kwa magoli 4-0, uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala.

Magoli ya JKT Queen yalifungwa na Fatuma Selemani aliyefunga hat trick mnamo dk 54,80 na 81,huku Zena Rashid akifunga dk 67.

No comments:

Post a Comment