Wednesday 12 August 2015

Tiketi tamasha la muziki la Party in the Park zanunuliwa kama njugu za Mil. 1.5 zamalizika

*Tiketi zilizobaki sasa ni za sh. 60,000 na 25,000

Jukwaa jipya litakalotumika katika tamasha hilo likijengwa kwa ajili ya majaribio kabla ya kuhamishiwa kwenye viwanja vya Farasi nyuma ya shule za Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
MAANDALIZI ya tamasha kubwa la muziki la Party in the Park litakalofanyika Jumamosi na kuwashirikisha wasanii wa Tanzania, Kenya na Afrika Kusini yamepamba moto huku tiketi zikinunuliwa kama njugu.

Tamasha hilo la aina yake litafanyika kwenye viwanja vya Farasi au The Green nyuma ya shule ya msingi na sekondari ya Oysterbay katika barabara ya Kenyatta.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mratibu wa tamasha hilo, Harry Magere alisema kuwa tayari wameanza kufunga jukwaa na maandalizi mengine ili kuhakikisha onesho hilo linafana.
Magere akizungumzia kiingilio alisema tayari tiketi za sh. Milioni 1.5 zimeshamalizika, ambapo meza moja itakuwa na viti sita na mteja wa meza hiyo atakuwa na mahali maalum pakuegesha gari lake.

Mbali na nafasi ya kuegeshea gari moja, pia watakaokaa katika meza hiyo watapewa chakula na vinywaji vya kuanzia.
Wanamuziki wa Tanzania, Alikiba na Feza Kessy walipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo.
Alisema kuwa mtu akayekaa katika viti vya VIP atalipia sh. 60,000 na sehemu ya kawaida sh.25,000 kama atanunua kabla ya tamasha hilo Jumamosi, lakini akinunua mlangoni siku ya onesho mtu wa VIP atalipa sh. 100,000 na yule wa sehemu ya kawaida atalipa sh. 30,000.

Alisema kuwa maandalizi yote yanakwenda vizuri na wanamuziki wa Sauti Sol kutoka Kenya watawasili Ijumaa asubuhi wakati wale wa makundi ya Afrika Kusini wanatarajia kuwasili siku hiyo usiku tayari kwa shoo hiyo kabambe.

Wasanii wa Afrika Kusini waliomo katika ratiba hiyo ya kutumbuiza katika tamasha hilo ni kutoka makundi ya Mafikizolo, Beatenberg na Black Motion wakati baadhi ya wasanii wa Tanzania watakuokuwepo ni Alikiba, Feza Kessy na wengineo.
Mtaalam wa Menu wa Eaters Point, Given Sandy (kulia) akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni kuhusu tamasha hilo kwa upande wa vyakula. Kushoto ni Meneja Masoko wa Benki ya KCB, Edgar Masatu, ambao ni miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo.
Aidha, Given Sandy akizungumzia kuhusu misosi siku hiyo alisema wamejipanga vizuri na wapenzi wa muziki watarajie kupata pizza za uhakika zenye viwango vya kimataifa.

Sandy ambaye ndiye meneja wa Eaters Point, ambazo ni mahiri kwa misosi alisema kuwa, timu yake imejipanga vizuri kwa ajili ya kutoa huduma katika tamasha hilo la kimataifa.

Wadhamini wa tamasha hilo ni pamoja na Peps, KCB Bank, Eaters Point, Wantanshi, East Africa TV na Radio, Savanna
Alikiba akizungumza na waandishi wa habari akiwa na mratibu wa tamasha hilo, Harry Magere Eaters Point maeneo ya Namanga barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

No comments:

Post a Comment