Sunday, 9 August 2015

Mo Farah ataka majibu ya wanariadha wanaopimwa kutumia dawa za kuongeza nguvu yawekwe hadharani ili kukomesha tabia hiyoMwanariadha wa Uingereza, Mo Farah akionesha medali zake za Olimpiki.

LONDON, England
BINGWA mara mbili wa Olimpiki Mo Farah, amesema kuwa anataka majibu ya wachezaji wanaopimwa kama wanatumia dawa za kuongeza nguvu, yawekwe hadharani.

Farah ametaka majibu ya vipimo hivyo hadharani, huku awali akisema: 'Nimefurahia kufanya kile kitakachodhihirisha kuwa mimi ni mwanariadha safi.'

Wiki iliyopita lilidai pamoja na Shirika la Utangazaji la Ujerumani kuwa lilifanya uchunguzi katika vipimo 12,000 kutoka kwa wanariadha 5,000 na kubainisha kuwa upo udanganyifu mkubwa kutoka mwa wanariadha wanaoshiriki katika mashindano makubwa duniani.

Wanariadha wiki iliyopita walipinga matokeo ya vipimo vyao kuwekwa hadharani.
yao ya vipimo kuwekwa hadharani.

 Farah, ambaye kocha wake, Alberto Salazar amekuwa akisakamwa kuhusu tuhuma za dawa za kuongeza nguvu, tangu wakati huo amekuwa akikanusha madai hayo yaliyotangazwa na kipindi cha Panorama Juni, ikiwatuhumu wanariadha wakubwa wa Uingereza kutumia dawa hizo na kukitaka Chama cha Riadha cha nchi hiyo kutoa maelezo kuhusu tuhuma hizo.

No comments:

Post a Comment