Friday 14 August 2015

Wasanii Sauti Sol watua leo Dar kwa kishindo, kutumbuiza kesho Jumamosi



Kundi la Sauti Sol likiimba kibao cha Sura Yako, mara baada ya kutua leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kundi hilo kesho Jumamosi litatumbuiza kwenye viwanja vya Farasi nyuma ya shule ya msingi Oysterbay, Dar es Salaam.
Na Seba Nyanga
KUNDI mahiri la muziki nchini Kenya la Sauti Sol jana liliwasili nchini tayari kwa onesho kabambe la muziki la Party in the Park litakalofanyika kwenye viwanja vya Farasi nyuma ya shule ya Oyesterbay jijini Dar es Salaam.

Kundi hilo lilitua kwenye Uwanja wa Mwalimu Nyerere saa 3:15 kwa ndege ya Kenya Airways na baadae kuimba kibao cha `Sura Yako Nzuri mara walipotoka nje ya uwanja ambako walikutana na waandishi wa habari.
 
Akzungumza na waandishi wa habari wanamuziki hao walisema kuwa, wamekuja kutoa shoo ya kufa mtu, ambapo waliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuwashuhudia.

Msanii mmoja wa kundi hilo Savara Mudigu alisema kuwa wamejipanga vizuri na kuwataka wapenzi wa muziki kufika kushuhudi makali yao kikiwemo kibao chao cha `Sauti Yako Nzuri ambacho kinapigwa sana na vituo mbalimbali vya radio na Tv hapa nchini.
 
Mwanamuzikimwingine wa kundi hilo, Polycarp Otieno alisema kuwa hii itakuwa mara yao ya nne kupiga muziki nchini Tanzania na ni mara yao ya tatu kupiga jijini Dar es Salaam na mara moja waliwahi kupiga Mwanza.

Aliwataka wapenzi wa muziki kukaa mkao wa kula kwani wamejipanga vizuri kungara katika tamasha hilo litakaloshirikisha pia makundi ya Afrika Kusini na Tanzania.

Wanamuziki wa Tanzania watakaofanya vitu katika tamasha hilo ni Ali Kiba pamoja na Feza Kessy wakati makundi ya Afrika Kusini ni pamoja na Mafikizolo, Beatenberg na Black Motion.

No comments:

Post a Comment