Saturday, 8 August 2015

Simba yasheherekea vizuri siku yao kwa kuifunga Club Sports Villa 1-0Mfungaji wa bao pekee la Simba leo kwenye Uwanja wa taifa dhidi ya Club Sports Villa ya Uganda, Awadh Juma (kushoto) akikimbia kushangilia pamoja na Mganda Simon Sserunkuma.

Na Mwandishi Wetu
SIMBA ya Tanzania jana ilisherehekea vizuri siku yao (Simba Day), baada ya kuifunga Club Sports Villa ya Uganda 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa mahsusi za kuhitimisha wiki ya Simba Day, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Singida Mjini anayemaliza muda wake, Mohamed Dewji. Dewji hivi karibuni alitangaza kutogombea kiti hicho tena.

Ushindi huo ni mwanzo mzuri kwa kocha Muingereza Dylan Kerr ambaye hivi karibuni alilalamikia ubutu wa safu yake ya ushambuliaji timu hiyo ilipokuwa kambini Zanzibar, ambako ilicheza mechi kadhaa za kirafiki.

Bao hilo pekee lilifungwa na Awadhi Juma katika dakika ya 90 ya mchezo huo baada ya kutokea piganikupige langoni mwa Club sports Villa.

Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi lakini jitihada zao za kusaka bao zinakwamishwa na Hamisi Kiiza ambaye alishindwa kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 13 baada ya kupata nafasi nzuri lakini anachelewa kufanya maamuzi na beki wa Club Sports Villa, Mbowa Paul anauokoa.

Villa wanajibu mapigo katika dakika ya 17 wakati Achema Robert anakuwa katika nafasi nzuri ya kufunga, lakini anapaisha mpira nje ya lango.

Dakika ya 23 Simba iliendelea kukosa mabao wakati Mussa Mgosi akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga, alipiga mpira nje.

Dakika mbili baadae, Kiiza alipata mpira lakini kabla ya kulifia lango, mpira huo unazuiwa na beki mmoja wa Villa.

Villa ilipata pigo baada ya mchezaji wao, Waibu Yesenikutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea Ibrahim Ajibu.

Dakika ya 55 Simba wanakosa tena bao wakati Mgosi lakini anapiga shuti linalodakwa kirahisi na kipa wa Club Sports Villa, Odongo Steven, huku Mohamed Hussein akipiga shuti nje ya 18 na kutoka nje ya lango.

Kikosi Simba: Vicent Angban, Ramadhani Kessy/Emiry Nimuboma, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Justuce Majbva/Haji Nuhu, Said Ndemla, Ibrahim ajibu/Mwinyi Kazimoto,Hamisi Kiiza, Mussa Mgosi na Peter Mwalyanzi/Simon Sserunkuma.

No comments:

Post a Comment