Friday, 14 August 2015

Pellegrini kumpa mkono Jose Mourinho timu zao zitakapocheza JumapiliKocha wa Man City, Manuel Pellegrini.

LONDON, England
KOCHA Mkuu wa Manchester City Manuel Pellegrini anasisitiza kuwa atampa m,kono jirani yake kocha wa Chelsea Jose Mourinho wakati timu hizo zitakapokutana Jumapili.

Chelsea ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya England watasafiri hadi kwenye Uwanja wa Etihad katika mchezo wa kwanza kati ya wapinzani hao wa taji katika msimu wa mwaka 2015-16.

Mahusiano kati ya Pellegrini na Mourinho yamekuwa sio mazuri, ambapo kocha huyo wa Chile akikataa kimpa mkono mpinzani wake huyo kufuatia Chelsea kushinda 2-1 Oktoba mwaka 2013.

Hatahivyo, kocha huyo wa City hana mpango wa kurudia kitendo hicho, ambapo aliwaambia waandishi wa habari: "Nina tofautiana naye lakini wakati wote nitampa mkono. "
Kocha wa Chelsea,Jose Mourinho
Man City inatarajia kuwa na mfungaji bora wa msimu uliopita, Sergio Aguero, katika mchezo huo, ambapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina hakucheza muda wote wakati timu hiyo iliposhinda 3-0 dhidi ya West Brom Jumatatu.

Pellegrini alingeza: "Sergio alifanya mazoezi kwa wiki nzima bila ya tatizo lolote kwea wiki yote.

"Labda hayuko fiti kwa asilimia 100 kwa sababu ni bora kwa mchezaji kucheza wakati wa mapumziko marefu ya kabla ya kuanza kwa ligi na sasa tuko tayari kwa Ligi Kuu na Sergio hana tatizo."


No comments:

Post a Comment