Monday, 24 August 2015

Mgombea wa Ukawa Edward Lowassa apanda daladala kutembelea wananchi Dar

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), anaeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa akilipa nauri ya daladala alilopanda Kituo cha Gongolamboto mwisho kuelekea Chanika,jijini Dar es Salaam leo alipokuwa kwenye  ziara ya kujionea hali halisi ya shida ya usafiri wa umma (daladala) jijini humo.

Lowassa akishuka kituo cha chanika na kupokelewa na Mgombea mwenza, Juma Haji Duni.
 Akipanda daladala

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na Bi. Kulwa Juma, anaejishughulisha na biashara ya kuuza Mihogo ya kukaanga katika Kituo cha Daladala cha Gongo la Mboto mwisho, jijini Dar es salaam leo, Agosti 24, 2015.

Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema ambaye anaungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya wananchi, UKAWA, Edward Lowassa leo ametembelea maeneo ya gongo la Mboto na kuzungumza na wananchi kadhaa akitumia usafiri wa daladala.

No comments:

Post a Comment