Monday, 24 August 2015

Mashindano ya dunia ya riadha yanavyoendelea Beijing, China kwenye Uwanja wa Taifa

Mwanariadha wa Algeria, Abdelhamid Zerrifi (juu), akichuana katika mchujo wa mbio za mita 3,000 kuruka gogo maji kwa wanaume katika mashindano ya dunia jijini Brijing, China kwenye Uwanja wa Taifa, maarufu kama `Tundu la Ndege'.  
Mwanariadha akianguka wakati wa mbio za mita 3,000 kuruka gogo na maji wakati wa mashindano ya dunia yanayoendelea Beijing, China.
Mchina Li Jinzhe akichuana katika raundi ya kufuzu kwa mchezo wa kuruka chini kwa wanaume katika mashindano ya dunia ya riadha kwenye Uwanja wa Taifa Beijing, China unaojulikana kama Kiota cha Ndege.
Mmarekani Michelle Carter akichuana katika fainali ya kutupa tufe kwa wanawake wakati wa mashindano ya dunia ya riadha yanayoendelea Beijing, China kwenye Uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment