Tuesday 25 August 2015

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Afariki Dunia, kuzikwa leo kwao Bukoba Mjini



MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA


TANGAZO LA KIFO



         Hayati Mhandisi Lambert W. Ndiwaita


Bodi  ya Ushauri, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wanasikitika  kutangaza kifo cha  Mwenyekiti wa Bodi  ya TAA,   Inj. Lambert W. Ndiwaita  kilichoteka  tarehe 20/08/2015  katika  Hospitali  ya Nairobi,  Kenya.  Marehemu anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake mjini Bukoba  tarehe 25/08/2015.

Mhandisi  Lambert Ndiwaita (64)  ni mmoja wa wataalamu waliobobea katika masuala ya  usafiri wa anga  kitaifa na kimataifa, katika kipindi cha uhai wake ametoa mchango mkubwa katika  maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini na nchi  nyingine duniadi.

Alianza shughuli zinazohusiana na  usafiri wa anga mwaka 19971  alipoajiriwa na iliyokuwa  Wizara ya  Ujenzi  kama  Mhandisi  Msaidizi na baadaye alipanda hadi   kufikia cheo cha  Mhandisi Mkuu  (Chief Engineer) akishughulikia masuala ya baeabara na  viwanja vya ndege. Mwaka 1993 alikwenda kufanya kazi katika Idara ya Usafiri wa Anga nchini Botswana kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mwaka 1994 aliajiriwa na  Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga  International Civil Aviation Organization (ICAO)  kusimamia  masuala ya  viwanja vya ndege (Aerodrome & Ground Aids) kwa eneo  la Mshariki na kusini mwa Afrika, katika ofisi za ICAO  zilizopo jijini Nairobi, Kenya.

Mhandisi Ndiwaita ni msomi aliyehitimu Shahada ya kwanza ya Uhandisi (Bsc Civil Engineering) katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Mwaka 1978 alihitimu  masomo Shahada ya Uzamili (Msc in Civil Engineering) katika Chuo kikuu cha Califonia, Berkley, nchini Marekani akijitikita zaidi katika masuala uhandisi wa ujenzi wa viwanja vya ndege.

Marehemu Lambert Ndiwaita atakumbukwa  na  wadau wa usafiri wa anga nchini na duniani kwa  mchango  mkubwa katika  maendeleo ya sekta hiyo  ambapo  kwa hapa nchini akiwa  Mwenyekiti wa Bodi  ya TAA  amechangia   kufanikisha ujenzi na uboreshaji wa viwanja  kadhaa  vikiwemo Mwanza, Tabora, Kigoma, Songwe,Mafia, Mpanda, Bukoba na Julius Nyerere  (JNIA).

Mungu ailaze roho marehemu  mahala pema peponi.

Imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu-TAA.
24th AUGUST, 2015
Agosti 12, 2015

No comments:

Post a Comment