Sunday, 9 August 2015

Japan wakumbuka miaka 70 kwa Nagasaki kulipuliwa na bomu la Atomic na kuuwa watu 70,000Mmoja wa manusurika wa bomu hilo la atomic miaka 70 iliyopita na kuuwa wato 70,000.

TOKYO, Japan
KUMBUKUMBU ya majonzi ilitawala katika mji wa Japan wa Nagasaki ambako ndege ya Marekani iliangusha bomu la atomic miaka 70 iliyopita.

Hotuba mbalimbali zilizotolewa wakati wa hafla hiyo zilimkosoa Waziri Mkuu aliyehudhiria Shinzo Abe kutokana na mipango yake ya kulegeza masharti ya jeshi la Japan.

Angalau watu 70,000 waliuawa katika shambulio hilo, ambalo lilitokea siku tatu baada ya kulipuliwa kwa bomu jingine huko Hiroshima.

Nagasaki ililipuliwa baada ya eneo lililopangwa awali kulipuliwa na Kokura, ambalo walishindwa kulifikia kutokana na mawingu kutanda.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni kutoka nchi 75 duniani, akiwemo balozi wa Marekani, Caroline Kennedy, ilianza Jumapili kwa kusomwa azimio lililosomwa na watoto.

Kimya cha dakika moja na kengele zililia wakati wa kuadhimisha mlipuko huo uliotokea mwaka 1945 saa 8:02.

Baadae Meya wa Nagasaki Tomihisa Taue alihutubia azimio la amani katika hafla hiyo. 

Aliyenusurika na shambulio la Nagasaki, Sumiteru Taniguchi, mwenye miaka 86 alielezea maumivu aliyoyapata akisema kuwa akubaliani na maelezo ya Bw. Abe.

No comments:

Post a Comment