Sunday, 18 June 2017

Ureno yatangaza siku tatu za maombolezo kufuatia vifo vya watu 61 walioteketea kwa moto mkubwa

LISBON, Ureno
URENO imetangaza siku tatu za maombolezo kufuatua watu 61 kufa kwa moto ikiwa ni moja ya janga kubwa la moto kuwahi kutokea nchi humo.

Watoto wanne ni miongoni mwa waliokufa, ambapo wengi wao walikutwa wamekufa ndani ya magari yao wakati wakijaribu kukimbia kutoka katikati ya mkoa wa Pedrógão Grande.

Mamia ya watu wa zima moto bado wanaendelea kupambana na moto huo unaoendelea kuwaka.

Waziri Mkuu Antonio Costa ameuta moto huo kuwa ni janga kubwa ambao limewahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.

Watu watano wa vikosi vya uokoaji inasemekana kuwa nao ni miongoni mwa watu waliofariki katika moto huo.

Watu wanne wa zima moto wenyewe wameumia wakiwa ni miongoni mwa watu 54 waliungua na moto huo ulionea katika eneo la milima ikiwa ni kilometa 200 kaskazini-mashariki na mji mkuu wa Lisbon.

No comments:

Post a Comment