Wednesday 14 June 2017

Tamthilia ya Huba yarejea kwa kishindo DStv


Na Mwandishi Wetu
Ile tamthilia kabambe ya Huba inayoonyeshwa kupitia DStv katika chanel ya Maisha Magic Bongo inaendela tena baada ya kumalizika kwa msimu wa kwanza wa tamthilia hiyo mwezi Machi mwaka huu. 

Huu ukiwa ni msimu pili, tamthilia hiyo ambayo imeainishwa kama moja ya tamthilia maarufu zaidi ukanda wa Afrika Mashariki, imeanza kwa kishindo kutokana na kuongezwa kwa vionjo na pia washiriki maarufu wa filamu hapa nchini.

Tamthilia ya Huba huigizwa hapa nchini na waigizaji wa hapa hapa nchini,  akiwemo  Rammy Gallis (Dev), Riyama Ali, Muhogo Mchungu, Grace Mapunda (Tesa) na Aunt Ezekiel (Jojo) ambaye ni muigizaji mpya katika tamthilia hii.

Akizungumzia ujio wa msimu wa pili wa Huba, Mkuu wa  chaneli ya Maisha Magic Bongo  Barbara Kambogi  amesema tangu kuanza kwa tamthilia hiyo ya Huba Mwezi Novemba mwaka jana imefanikiwa kuliteka soko la tamthilia hapa Afrika Mashariki na kuifanya kuwa moja ya tamthilia matata kabisa katika soko la Afrika Mashariki.

“Kwa mara ya kwanza katika historia ya filamu na hususan tamthilila Watanzania tumefanikiwa kuiweka tasnia yetu ya uigizaji filamu katika ramani ya kanda ya Afrika Mashariki na bara zima kwa ujumla kutokana na ufanisi wa tamthilia yetu ya Huba ambayo inatayarishwa hapa nchini na kuigizwa na watanzania wenyewe” alisema Barbara.

Amesema kuwa kwa ufanisi uloonyeshwa na tamthilia hiyo katika msimu wa kwanza, wanatarajia kuwa msimu huu wa pili utakuwa wa kuvutia zaidi hasa ikizingatiwa kuwa waigizaji wote wameiva vizuri zaidi, vionjo vimeongezwa na pia waigizaji wengine wapya akiwemo Anti Ezekiel ambaye ni miongoni mwa waigizaji maarufu hapa nchini.
“Sisi DStv, na hususan channel yetu ya Maisha Magic Bongo, tulisikia kilio cha muda mrefu cha Watanzania wengi waliokuwa wakitutaka kuongeza maudhui ya Kitanzania, na hatimaye tukaamua kuanzisha chaneli maalum yenye maudhui kutoka Tanzania. Na sasa tunaendelea kuiboresha chaneli hii ya Maisha Magic Bongo na maudhui yake kwa ujumla hivyo watanzania wasiache kutazama chanel hii kwani ni yetu” alisema Barbara.

Tamthilia ya Huba katika chanel ya Maisha Magic Bongo inapatikana katika vifurushi vyote vya DStv kikiwemo kile cha DStv Bomba kwa shilingi 19,975 tu kwa mwezi kikiwa ni moja ya vifurushi vya bei nafuu kabisa sokoni.

Msimu huu wa pili wa huba unatarajiwa kuendelea kwa miezi kadhaa  na tamthilia hiyo huoneshwa katika chanel ya Maisha Magic Bongo (DStv 160) kila siku za Jumanne na Jumatano saa moja na nusu usiku.

No comments:

Post a Comment