Friday 16 June 2017

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege yatembelea vitengo vyake wiki ya Utumishi wa Umma

Na Mwandishi Wetu
MAKAO Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imejionea shughuli za uendeshaji za vitengo vyake katika siku ya kwanza ya Wiki ya Utumishi wa Umma, ambayo itamalizika Juni 23.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Ramadhan Maleta jana alijionea shughuli hizo zinazofanywa na vitengo vya mamlaka hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Ramadhan Maleta akiteta na Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA), Joseph Nyahende (kushoto) wakati wa  kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma leo. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu.
Akizungumza na wakuu wa vitengo katika ofisi ya Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam (JNIA), Maleta alisema kuwa tofauti na miaka mingine, mwaka huu wiki hiyo inaazimishwa kwa kutembelea vitengo mbalimbali ili kujua uendeshaji wake, changamoto na jinsi wanavyopambana nazo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Ramadhan Maleta akiteta na Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA), Joseph Nyahende (kushoto) wakati wa  kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma leo. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu.
Ofisa Biashara wa JNIA, Herrieth Nyarusi akizungumza wakati Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Ramadhan Maleta alipotembelea uwanja huo leo kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. Kulia ni Meneja wa Fedha, Shadrack Chilongani na Godfrey Kanyama.
Alisema utaratibu huo umetolewa na serikali badala ya kufanya maonesho kwenye Uwanja wa Taifa au katika viwanja vya ofisi mbalimbali, mwaka huu wiki hiyo inaanzimishwa kwa wakuu kutembelea idara mbalimbali na kujionea utendaji wa kazi na changamoto zinazowakabili.

Maleta alipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa JNIA, Joseph Nyahende ambaye alieleza wanavyoendesha shughuli zao kuanzia kuwahudumia abiria na mambo mengine mengi.
Pia Maleta alitembelea vitengo vya usalama katika eneo la kuwasili na kuondokea abiria maarufu au VIP, ambako alipata maelezo kutoka kwa mkuu wa usalama, Leonard Mbogom na kitengo cha uhasibu na kupata maelezo kutoka kwa mhasibu msaidizi, Easter Mwigane

Msafara huo pia ulipitia katika vitengo vya Usalama, eneo la kuondokea abiria katika Uwanja wa JNIA Terminal Two, kitengo cha makusanyo na kile cha usalama kwenye uwanja huo.
Kitengo cha usalama kimekuwa na shughuli nyingi, ambapo kimekuwa kikiweka kumbukumbu za idadi na muda wa ndege zilizotua na kupaa na usalama mzima wa kiwanja na mambo mengine mengi.

Maleta alishukuru idara zote na kuzitaka kujitahidi kutatua changamoto zinazowakabili, ambapo Jumatatu atakutana na wafanyakazi wote kuzungungumzia mambo mbalimbali zikiwemo kero.


 

 

No comments:

Post a Comment