Thursday 8 June 2017

Taifa Stars kukipiga na Lesotho Usiku Chamazi

Na Mwandishi Wetu
MCHEZO wa kwanza wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya wenyeji, Tanzania, Taifa Stars,  na Lesotho, Mamba, utachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Jumamosi kuanzia Saa 2:00 usiku.

Rais wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema jana usiku kuwa, mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Chamazi ulioko Mbagala.

Amesema kuwa sababu kubwa ya mchezo huo kufanyika Uwanja wa klabu ya Azam ni kutokana na Uwanja wa Taifa kuwa katika marekebisho madogo.

Rais Malinzi amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Jumamosi Azam Complex, kuishangilia timu yao ili iweze kufanya vizuri.

Taifa Stars itaingiaa kwenye mchezo huo ikitoka kwenye kambi ya wiki moja mjini Alexandria, Misri.

Nahodha Mbwana Ally Samatta hakuwepo Misri na anatarajiwa kuungana na wenzake hapa Dar es Salaam akitokea Ubelgiji ambako anachezea klabu ya KRC Genk.


Kiungo wa DC Tenerife ya Hispania, Farid Mussa na mshambuliaji wa AFC Eskilstuna ya Denmark, Thomas Ulimwengu wao walikuwepo Misri na wako tayari kwa mchezo wa Jumamosi.

No comments:

Post a Comment