Sunday, 11 June 2017

Umisseta taifa yazidi kupamba moto Mwanza

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
TIMU za wasichana za mpira a kikapu za Mwanza na Kilimanjaro zimeendelea kutamba katika Michezo ya Shule za Sekondari inayoendelea mjini haa baada ya kutoa vichapo kwa wainzani wao.

Mwanza waliifunga Tabora kwa pointi 66-20, katika mchezo uliofanyika kenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba jana Jumamosi.

Timu ya Mkoa wa Kigoma wenyewe waliibuka washindi baada ya kuwashinda wainzani wao kwa vikapu 20-14 wakati Katavi ilisambaratisha Tabora kwa vikapu 36 kwa 28 huku Simiyu ilipoteza kwa vikapu 12 dhidi ya 14 vya Mtwara.

Kwa upande wa timu za wavulana, Iringa alijikuta akiokea kichapo cha pointi 20-14 kutoka kwa Dodoma huku Kilimanjaro ikitamba dhidi ya Njombe kwa vikapu 54-42,

Mtwara ilishinda 38-25 dhidi ya Ruvuma wakati Pemba ilifunga Pwani kwa vikapu 33-32 huku Morogoro ikiisambaratisha Simiyu kwa vikapu 59-03.Tanga iliifunga Katavi 25-9 na Mara ilifungwa na Ruvuma vikapu 34-33.

Kwa upande wake mratibu mkuu wa mchezo wa mpira wa kikapu Haidari Abdul alisema michezo hiyo inaendelea vizuri na vijana wanajitahidi kucheza kwa kujituma.

Alisema wadau mbali mbali wajitokeze kwa wingi katika kuhakikisha wanakuja  kuchagua wachezaji wenye vipaji ili kukuza mchezo huo hapa nchini.

Katika mchezo wa mpira wa wavu upande wa wavulana,Tanga ilifunga Arusha kwa seti 3-0, Geita 3 iliifunga Morogoro seti 3-0 na Pwani ikaifumua Kigoma 3-0.

Kwa upande wa mchezo wa soka, timu ya Unguja ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya huku bao hilo ekee likifungwa na Ibrahim Hamad.


Unguja ndio inayoongoza katika msimamo wa Kundi C ikiwa na pointi 12.

No comments:

Post a Comment