Na Mwandishi Wetu
MSHINDI wa kwanza wa mbio za pili za Kimataifa za Kil FM nusu marathon
zitakazofanyika Agosti 13 mjini Moshi, ataondoka na kitita cha sh 700,000,
imeelezwa.
Mwaka jana mbio hizo zilifanyika kwa mara ya kwanza mjini Moshi na
kushirikisha zaidi ya wakimbiaji 2,000 kutoka ndani na nje ya nchi.
Akizungumza jana mratibu wa mbio hizo, Nelson Mrashani alisema kuwa,
mshindi wa kwanza ataondoka na kitita hicho wakati yule wa pili atatia
kibindoni sh 500,000.
Alisema kuwa bado wanakaribisha wadhamini kujitokeza kusaidia kufanyika
kwa mafanikio mbio hizo, ambapo mshindi watatu atabeba sh 300,000 huku wa nne
ataondoka na sh 200,000 na watano sh 100,000.
Mrashani alisema kuwa mshindi wa sita hadi wa 10, kila mmoja atapata
kifuta jasho cha sh 50,000 huku washindi wa mbio za kilometa tano za
kujifurahisha, hawatakuwa na zawadi.
![]() |
Mratibu mkuu wa mbio za kimataifa za Kili FM Marathon, Nelson Mrashani akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
|
Alisema kuwa mshindi wa kwanza katika mbio za watoto za kilometa 2.5,
ataondoka n ash 50,000 huku mshindi wa pili 30,000, watatu 20,000 na wanne na
tano kila mmoja atapewa sh 10,000.
Zawadi hizo zote kuanzia zile za nusu marathon pamoja na zile za kilometa
2.5 zote ni kwa wanawake na wanaume na wavulana na wasichana.
Mrashani alisema kuwa waandaaji wa mbio hizo wanatarajia kuboresha zaidi
katika pande zote na wanatarajia washiriki wengi kujitokeza.
No comments:
Post a Comment