Friday, 16 June 2017

Ronaldo ataka kuondoka Real Madrid

MADRID, Hispania
CRISTIANO Ronaldo anataka kuondoka Real Madrid kwa sababu hataki tena kucheza soka Hispania, imeelezwa.

Winga huyo wazamani wa Manchester United amechukizwa na jinsi mamlaka ya mako nchini humo yanavyomsakama na sasa anataka kuondoka nchini humo.

Waendesha mashtaka wa Hispania walimtuhumu mchezaji huyo kukwepa kodi ya Euro milioni 15, mashtaka ambayo Ronaldo ameyakana vikali.

Ronaldo alisaini mkataba wa miaka mitano Novemba mwaka jana ikiwa na maana atakuwa katika klabu hiyo hadi 2021.

Tayari kumekuwa na nia kutoka China wakati msimu wa katikati wa usajili ukitazamiwa kuanza Jumatatu.


Nahodha hiyo wa Ureno anakabikiwa na mashtaka manne ya kukwepa kodi katika mahakama ya mkoa ya Madridi kutoka kwa mwendesha mashtaka wa serikali ikiwa ni pamoja na haki ya malipo ya matumizi ya picha yake.

No comments:

Post a Comment