![]() |
Jengo la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Terminal 3 likionekana kwa nje leo. |
Na Mwandishi Wetu
UJENZI wa jengo la kuondokea na kuwasili abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
cha Julius Nyerere (JNIA) Terminal 3 utakamilika Septemba mwakani na kuanza
kutumika rasmi miezi mitatu baadae, imeelezwa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa aliyasema hayo leo baada ya
kukamilisha ziara ya kutembelea jengo la kiwanja hicho, ambalo ujenzi wake
unaendelea.
Mbarawa alisema kuwa, ujenzi huo unaendelea vizuri na utakamilika Septemba
2018 na kuanza rasmi kutumika Desemba mwaka huo huo.
![]() |
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na wafanyakazi kabla ya kutembelea Jengo la Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere Terminal 3 leo. |
Alisema jengo hilo litakakuwa likichukua jumla ya abiria milioni 6 kwa
mwaka tofauti na jengo lile la Terminal Two, ambalo lina uwezo wa kuchukua
abiria milioni 2 tu kwa mwaka, hivyo majengo hayo mawili yakakuwa yakichukua
jumla ya abiria milioni 8 kwa mwaka.
Alisema kuwa hatua ya kuchukua abiria wengi litasaidia kuongeza watalii
wanaotembelea vizutio vilivyopo nchini.
![]() |
Waziri Profesa Mkame Mbarawa akisaini kitabu cha wageni leo. |
Aliongeza kuwa eneo la maegesho ya kiwanja hicho yatakuwa yakichukua
jumla ya ndege 21 kwa wakati mmoja, hivyo kuwezesha watu wengi wakiwemo watalii
kuja nchini kupitia katika kiwanja hicho cha ndege.
Pia Mbarawa alimuhakikishia mkandarasi wa uwanja huo kuwa, atalipwa fedha
zake zote kwa wakati kama alivyoahidi Rais John Pombe Magufuli alipotembelea
kiwanja hicho mapema mwaka huu.
Mbarawa alitembelea maeneo mbalimbali ya jengo hilo yakiwemo yale ya
kukaa abiria wanaondoka na kuwasili, vyumba vya wageni mashuhuri na sehemu
tofauti tofauti, ambazo zinajengwa kwa umahiri mkubwa.
Waziri Mbarawa alipata maelezo ya kina ya ujenzi huo kutoka kwa
mkandarasi, Simba Charles na Meneja Ujenzi, Ray Blumrick wa Kampuni ya
BAM-Unternational-Afrika.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa (wa pili kulia) akifurahia jambo na Mkandarasi Simba Charles alipokagua ujenzi wa jengo la Kiwanja kipya cha Ndege cha Kimatafa cha Julius Nyerere (JNIA) Terminal 3 leo.