MWEKA Hazina, William Mkombozi ‘Mgosi’ amerudi kwa kishindo katika
nafasi hiyo baada ya kushinda kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Michezo kwa
Idara na Wizara za Serikali (SHIMIWI), uliofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi
wa hoteli ya Mount Uluguru mkoani Morogoro.
Mkombozi aliyewahi kuongoza katika miaka ya mwanzoni ya 2000 akiwa na
aliyewahi kuwa mjumbe na baadaye Katibu Mkuu, Bw. Ramadhani Sululu, lakini
baadaye alikaa pembeni sasa amechaguliwa tena kwa kura 23.
Naye Alex Temba aliyeongoza kwa muda mrefu katika Klabu yenye wachezaji
mahiri ya Uchukuzi, alichaguliwa kuwa Katibu Msaidizi baada ya kushinda kwa
kura 28 na kumbwaga Margreth Mtaki aliyepata kura 15.
Hatahivyo, nafasi ya Mwenyekiti ilirudi tena kwa Daniel Mwalusamba
aliyekuwa hana mpinzani kwa kupata kura 42;
huku Ally Katembo akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kura 41;
wakati Moshi Makuka ametetea nafasi yake ya Ukatibu kwa kura 38 dhidi ya Andrew
Sekimweri aliyeondoka na kura sita.
Katika nafasi ya Mweka Hazina Msaidizi, ameshinda Frank Kibona kwa kura
21; wakati walioshinda kwenye ujumbe wa kamati ya utendaji na kura zao zikiwa
kwenye mabano ni Apolo Kayungi (44), Assumpta Mwilanga (42), Aloyce Ngonyani
(40), Damiani Manembe (39) na Seleman
Kifyoga (31).
Kwa upande wa nafasi ya viti maalum wanawake walioshinda ni Mwajuma
Kisengo (20) na Mariam Kihange (18) na waliwashindwa ni Costance Momadi (16) na
Buya Masunga (12).
![]() |
No comments:
Post a Comment