Na Mwandishi Wetu
Ndugu
Waandishi wa Vyombo vya Habari mbalimbali za Michezo,
Kwa mara
nyingine tumekutana tena ili tuweze kuwapa baadhi ya taarifa za shughuli ambazo
Kamati ya Olimpiki Tanzania huzifanya na kuzitekeleza kwa mujibu wa Katiba yetu
ya TOC.
Leo katika
muhadhara huu kwa niaba ya Kamati ya
Olimpiki Tanzania napenda kuchukua nafasi hii kuwaarifu mambo matatu (3) muhimu
ambayo mara kwa mara Waandishi mbalimbali wa Habari hasa za Michezo wamekuwa
wakiyauliza:
1. Taarifa ya
Uchaguzi Mkuu wa Kamati ya Olimpiki
Tanzania.
2.
Utambaulisho wa Kamisheni ya Kusimamia Uchaguzi wa
TOC.
3. Taarifa ya
Uchaguzi wa Kamisheni ya Wachezaji.
![]() |
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi. Kushoto ni Mhazini Mkuu wa TOC, Charles Nyange na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TOC, Irine Mwasanga.
|
a. Taarifa ya Uchaguzi wa TOC:
Uchaguzi huu ambao utafanyika mwaka
huu kwa
mujibu wa Katiba ya TOC (Ibara ya 20
Para 1)
utafanyika Dodoma Disemba 10, 2016.
Ufuatao ni utaratibu mzima wa Maandalizi ya
Uchaguzi wa
TOC:-
a. Uchukuaji wa Fomu za Wagombea zitaanza
kutolewa katika ofisi za TOC (Tanzania Bara na
Zanzibar) tarehe 25/10/2016
na kurejeshwa tarehe
15/11/2016
(Katiba ya TOC Ibara ya 23 para 2.)
b.
Ada ya Fomu ya Wagombea zitauzwa na ofisi ya
TOC (Bara na Zanzibar) kwa gharama zifuatazo:
i. 200,000.00 (Rais, Makamu wa Rais, Katibu
Mkuu, Katibu Mkuu Msaidizi, Mhazini Mkuu,
na
Mhazini Mkuu Msaidizi)
ii. 150,000.00 (Wajumbe)
c.
Kurejesha Fomu:
Fomu zitarejeshwa Ofisi Kuu na
Ndogo za TOC
zilizoko Mwananyamala, Jengo la
Shirika la Nyumba
la Taifa (Biashara Complex)
ghorofa ya tatu na
Uwanja wa Amani, Zanzibar tarehe 15/11/2016 kabla
ya saa 10.00 mchana. Fomu
hazitapokelewa baada
ya
tarehe na muda huo.
d.
Kuhakiki Fomu baada ya kurejeshwa:
18/11/2016: Kamisheni itakutana Dar Es
Salaam
ili kupitia na kuzihakiki fomu
zote tayari kwa usaili.
e. Usaili wa Wagombea:
Usaili wa Wagombea utafanyika:
i.
22/11/2016
(Dar Es Salaam, Tanzania)
ii. 24/11/2016 (Zanzibar, Tanzania)
Usaili utafanyika kwa lugha
ya Kiswahili na
Kiingereza.
f.
Kutangaza Matokeo:
Tarehe 30/11/2016: Kamisheni ya Uchaguzi itakutana
na Waandishi wa Vyombo vya Habari
katika ofisi ya
TOC Dar Es Salaam kutangaza
majina ya Wagombea
waliopitishwa.
g. Malalamiko:
Baada ya kutangazwa matokeo, kama kutakuwa na
malalamiko, yatapokelewa na kusikilizwa kuanzia
siku baada ya majina ya wagombea
yatakapotangazwa (30/11/2016).
h. MUHIMU:
i. Sifa
ya Mgombea:
Kama
ilivyooanishwa katika Katiba ya TOC (Ibara
ya 22 para 1-10).
ii.
Ikiwa mgombea jina lake halikupitishwa na
atahitaji
maelezo ya sababu za jina lake
kutopitishwa, Kamisheni ya Uchaguzi ina wajibu
wa kumfahamisha na kumridhisha mgombea
sababu za jina lake kutopitishwa.
Kila mgombea
atakayepitishwa ambaye siyo
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji inayomaliza muda wake atapaswa kujilipia gharama
zake zote za kwenda na kujikimu atakapokuwa Dodoma wakati wa uchaguzi
(10/12/2016).
1. Utambulisho
wa Kamisheni ya Kusimamia Uchaguzi wa
TOC.
Katika kikao chake cha tatu (3)
kilichofanyika Zanzibar
hapo tarehe 27/08/2016, Kamati ya Utendaji
ya TOC
ilipendekeza Kamisheni itakayosimamia
Utaratibu mzima
wa uchaguzi wa viongozi wa TOC kwa miaka 4
ijayo.
(Katiba
ya TOC, Ibara ya 21, Kipengele Na. 6)
Kamisheni hiyo ya watu watatu (3) ilikuwa na Wajumbe
wafuatao:-
a. Lloyd Nchunga-Tanzania Bara
b. Harrison Chaulo-Tanzania Bara
c. Abdallah Juma Mohamed-Zanzibar
Kamisheni hiyo
hapo juu itasimamia Maandalizi na Uchaguzi Mkuu wa TOC tu.
TAARIFA YA UCHAGUZI WA KAMISHENI YA WACHEZAJI TANZANIA
(KAWATA)
Uchaguzi huu
utafanyika mjini Dodoma tarehe 8/12/2016
siku mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu wa TOC.
Kamisheni ya
Wachezaji Tanzania (KAWATA) ilifanya uchaguzi wake mjin Dodoma tarehe
06/12/2012.
Ni matuimaini
ya Kamati ya Olimpiki Tanzania kwamba,
KAWATA Taifa imefanya kazi kubwa ya kuvihamasisha Vyama/Mashirikisho ya
Michezo kufanya chaguzi zao tangu kwa kufuata mwongozo wao.
KAWATA Taifa
iko chini ya Ulezi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, kama ilivyo Kamisheni ndani
ya Vyama/Mashirikisho ya Michezo kuwa chini ya ulezi wao
Vyama/Mashirikisho hayo.
Kwa muongozo
wa KAWATA, Kamisheni ya Taifa na Vyama/Mashirikisho ya Michezo inatakiwa kuwa
na Wajumbe wasiopungua 5 na kuzidi 8.
Nafasi
zitakagombewa:
1.
Mwenyekiti
2.
Katibu
3.
Wajumbe 4/6 (Kwa idadi sawa ya jinsia)
Fomu za
Wagombea zitatolewa na kurejeshwa tarehe 28/10/2016
na 11/11/2016 kabla ya saa 10.00 mchana katika ofisi za TOC
Tanzania Bara na Zanzibar.
Wagombea
ambao hawatakuwa Wajumbe wa Kamisheni ya Chama/Shirikisho la Mchezo husika
watakaohudhuria Mkutano Mkuu mjini Dodoma tarehe 8/12/2016 itawalazimu kujilipia
gharama ya kwenda Dodoma mara tu majina yaliyopitishwa yatakapotangazwa.
Maandalizi na Usimamizi wa Uchaguzi wa
KAWATA utafanywa na Sekretariat ya
Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).
No comments:
Post a Comment