Monday 24 October 2016

Fomu za kuwania uongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kuanza kutolewa kesho jijini Dar es Salaam na Zanzibar


Rais wa Kamati ya Olimpiki, TOC, Gulam Rashid akizungumza hivi karibuni. Kushoto ni Katibu Mkuu wake, Filbert Bayi.

Na Mwandishi Wetu
MBIO za kuwania uongozi katika Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) zinatarajia kuanza kesho Jumanne Oktoba 25 wakati fimu za kuwania uogozi zitakapoanza kutolewa tayari kwa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Dodoma Desemba 10 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi alisema jijini Dar es Salaam wiki iliyopita kuwa, fomu hizo zitaanza kutolewa Oktoba 25 na mwisho wa kurejeshwa ni Novemba 15 saa 10:00 jioni katika ofizi za kamati hiyo zilizopo Mwananyamala na ofisi ndogo ya Zanzibar.

Bayi alisema kuwa fomu za wanaotaka kugombea Urais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhazini Mkuu, Mhazini Msaidizi wachukua fomu kwa sh. 200,000 kila mmoja huku wanaotaka kuwania ujumbe watatakiwa kutoa sh 150,000.

Kamisheni ya Uchaguzi itakutana jijini Dar es Salaam na kuhakiki fomu zote Novemba 18 kabla ya kufanyika kwa usaili utakaendeshwa Novemba 22 jijini Dar es Salaam wakati Zanzibar utakuwa Novemba 24.

Alisema kuwa usaili huo utafanyika kwa lugha ya Kiswahili na kiingereza, kwani ndizo lugha za TOC, ambapo Bayi alisisitiza kuwa wagombea wanatakiwa kujua vizuri kugha hizo.

Alisema kuwa kila mgombea atakayepitishwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi ambaye sio mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TOC, atatakiwa kujigharamia zote za kwenda Dodoma, malazi na chakula akiwa huko.

Kamisheni ya Uchaguzi inaoongozwa na Lloyd Nchunga na Harrison Chaula (Tanzania Bara) na Abdallaj Juma Mohamed (Zanzibar).

Aidha, Bayi alisema kuwa Kamisheni ya Wachezaji Tanzania (Kawata) itafanya uchaguzi wake mjini Dodoma Desemba 6 siku mbili kabla ya ule wa TOC katika Hotel ya Dodoma.

No comments:

Post a Comment