Tuesday 18 October 2016

Wateja DStv kufaidi punguzo la vifurushi kuanzia Novemba Mosi, 2016



Na Mwandishi Wetu
WAPENZI wa michezo na burudani za aina mbalimbali kupitia kingamuzi cha DStv kuanzia Novemba mosi watafaidi uhondo huo kwa gharama nafuu, imeelezwa.
Meneja Uendeshaji wa Multchoice-Tanzania, Baraka Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu punguzo la bei za vifurushi vya king’amuzi chao.
Kwa mujibu wa meneja muendeshaji wa Multchoice-Tanzania Baraka Shelukindo, hatua hiyo imechukuliwa ili kuwapunguzia gharama wateja na kwa uhondo zaidi.

Shelukindo alisema kuwa wameamua kunufaisha wateja wake kwa kufanya mapinduzi makubwa kupitia punguzo la bei na kuongeza  chaneli 8  kupitia huduma yake ya DStv.
Meneja Mauzo wa Multchoice-Tanzania, Salum Salum akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Ofisa Rasilimali Watu, Tike Mwakitwange. Kushoto ni Ofisa Uhusiano Duphney Numoka na Meneja uendeshaji, Baraka Shelukindo.
Huduma hizo mpya za punguzo la bei zitaanza rasmi kufanya kazi kuanzia tarehe Novemba mosi, ambavyo ni DStv Premium, Compact Plus, Compact, Family na Access. 

DStv Premium  imefanya punguzo la asilimia 16, ambapo bei mpya sasa itakuwa sh 184,000 wakati bei ya zamani ni sh 219,000 wakati DStv Compact Plus, imepunguzwa kwa asilimia 17 na sasa itakuwa sh 122,500 (zamani 147,000) Compact ya kawaida sasa ni sh 82,250 wakati zamani ni sh 84,500.
Meneja Mauzo wa Multchoice-Tanzania, Salum Salum akizungumza na waandishi wa habari huku Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo, Baraka Shelukindo akimsikiliza.
Alisema sasa kifurushi cha familia, ambacho sasa kitakuwa sh 42,900 badala ya bei ya awali ya sh 51,000 kwa mwezi.

Kifurushi cha DStv Bomba kitafaidisha wateja wake kwa ongezeko la chaneli 3, na punguzo la asili mia 15, bei yake mpya ni sh 19,950. Punguzo hili la bei kwa kifurushi hiki litaanza Novemba 15.
 
Alisema kuwa wateja wataendelea kufaidi burudani ya hali ya juu ya vichekesho, tamthilia, sinema, michezo na vinginevyo kutoka katika kingamuzi cha DStv.

Chaneli hizo mpya zitakazorushwa ni Vuzu AMP, Lifetime, Discovery channel,Crime & Investigation, History channel na Africa Magic Showcase.
Waandishi wa habari wakiuliza maswali katika hafla hiyo ya kutangaza punguzo la bei za vifurushi vya DStv.

DStv Compact Plus, imeongezewa chaneli za michezo zitakazoendeleza msisimko kwa wapenzi wa mpira wa miguu kupitia  vipindi vya UEFA Champions Leagues, European Football leagues na Europa league. Hizo mechi zote zinapatikana kwenye stesheni za SuperSport 6 (SS6) na SuperSport 4 (SS4).

Kwa wapenzi wa filamu za kiafrika, watafaidi kupitia Nollywood , wapenzi wa tamthilia zakilatino  wataburudishwa na telenovelas pamoja na filamu za Bollywood.  Bila kusahau sinema zitakazopatikana kupitia chaneli za ROK, Eva Plus na B4U Movies.

No comments:

Post a Comment