Sunday, 9 October 2016

Nigeria, Misri, Tunisia zaanza vizuri mbio za kusaka nafasi ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2018Mchezaji wa Zambia, Rainford Kalaba (kulia) akitafuta njia kumpita mchezaji wa Nigeria, Ogeny Onazi wakati wa mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia Kanda ya Afrika uliofanyika Levy Mwanawasa jijini Ndola, Zambia jana. Nigeria ilishinda 2-1. Picha na Mtandao).

NDOLA, Zambia
NIGERIA imeanza kwa ushindi kampenzi zake za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 Kanda ya Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Zambia katika mchezo wa Kundi B uliofanyika hapa.
 
Kwa ushindi huo, Nigeria wanaoongoza katika kundi lao, baada ya vigogo wengine wa Afrika Algeria kubanwa na kulazimishwa sare na Cameroonin na kutoka sare ya kufungana bao 1-1.

Kwingine, Misri iliifunga Congo 2-1 katika mchezo wa Kundi E uliofanyika Brazzaville huku katika Kundi A, Tunisia ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Guinea.

Katika mchezo wa Nigeria, mabao yao yalipatikana katika kipindi cha kwanza yaliyofungwa na nyota wanaongara katika timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza.

Mshmabuliaji wa Arsenal Alex Iwobi ndiye aliyeiweka mbele Super Eagles baada ya kufunga bao katika dakika ya 32.

Mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho aliongeza uongozi huo wa City dakika 10 baadae na kukiweka kikosi cha kocha Gernot Rohr kuwa mbele kwa mabao 2-0.

Nigeria nusura ipate bao la tatu na ingeweza kuwa mbele kwa mabao 3-0 katika mchezo huo uliofanyika Ndola kama sio nahodha wake John Mikel Obi kukosa bao katika kipindi cha pili, baada ya kupiga shuti la mbali lililookolewa kifundi na kipa wa Zambia Kennedy Mweene.

Zambia ilipambana kiume na juhusi zake zilileta mafanikio pale ilipopata bao la kufutia machozi katika dakika ya 71 kupitia kwa Collins Mbesuma.

Pamoja na presha kutoka kwa timu mwenyeji, Nigeria iligangamala na kuendeleza rekodi ya ushindi ugenini na kuongoza katika Kundi B, likiwa ni moja ya makundi magumu katika mechi hizo za kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Timu nyingine mbili katika Kundi B, Algeria, ilimchezesha mchezaji wake anayekipiga Leicester City, Riyad Mahrez na Islam Slimani, wakati ikicheza na Cameroon na kutoka sare ya bao 1-1.

Muargeria El Arabi Soudani aliiweka mbele timu yake katika mchezo uliofanyika Blida, lakini yule wa Cameroon, Benjamin Moukandjo ilisawazishwa kabla ya mapumziko.

Pia katika mchezo mwingine uliofanyika Jumapili, Misri ilikwenda kileleni katika Kundi E kwa ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Congo Brazzaville, wakifuatiwa na suluhu ya Ghana nyumbani dhidiya Uganda katika mchezo uliofanyika Ijumaa.

Wenyeji waliuanza mchezo huo kwa nguvu wakati mchezaji wake anayecheza soka la kulipwa Ufaransa Ferebory Dore alipofunga bao la kuongoza kwa Congo Brazzaville katika dakika ya 24.

Hatahivyo, kikosi kabambe cha Misri kilijibu mapigo kwa mshambuliaji wake anayecheza soka la kulipwa Roma Mohamed Salah kusawazisha dakika nne kabla ya mapumziko na matokeo kuwa 1-1.

Katika dakika ya 58, Salah alibadili matokeo wakati alipomtengenezea mcherzaji wa Al Ahly, Abdallah El-Said aliyefunga na kufanya matokeo kuwa 2-1 kwa Misri.

Tunisia iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Guinea katika mchezo wa Kundi A huko Monastir uliofanyika baadae Jumapili.

Mabao ya kipindi cha pili kutoka kwa Aymen Abdennour na Ahmed Akaichi yaliipatia timu hiyo ya Afrika Kaskazini ushindi ulioiweka katika nafasi ya pili katika Kundi A, nyuma ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliyoifunga Libya 4-0 Jumamosi.

Washindi watano wa makundi ndio watakaofuzu kwa ajili ya kuliwakilisha bara la Afrika katika fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Urusi mwaka 2018.

No comments:

Post a Comment