Sunday, 23 October 2016

Tamasha la kwanza la Chakula na uvuvi wakati wa kumbukumbu ya Kilwa Jazz lafana Kilwa MasokoNa Mwandishi Wetu, Kilwa
TAMASHA la Kwanza la Chakula na Uvuvi lilikamilika leo usiku a maneno mjini Kilwa Masoko huku bendi ya La Rhumba ikipamba kwa kupiga nyimbo kibao zikiwemo zile za Kilwa Jazz Band.

Kwa mujibu wa mratibu wa tamaha hilo, ambaye pia ndiye mmiliki wa Kilwa Dreams Resort Hotel Gradys Rutihinda, tamasha hilo pia ni kwa ajili ya kupiga vita uvuvu haramu pamoja na kumuenzi mwanamuziki mkongwe nchini Hemed Kipande, ambaye alikuwa mwenyeji wa Kilwa Kivinje.
 
Rutihinda alisema kuwa pia tamasha hilo ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka ni kwa ajili ya kutangaza fursa za utalii na uchumi zilizopo Kilwa, ambazo wengi hawajui kama zipo.

Tamasha hilo limeanza kwa kishindo na kushirikisha watu kadhaa huku shindano la uvuvi likiwa kivutio baada ya timu ya Kilwa Dreams kuibuka washindi baada ya kumvua samaki mwenye uzito wa kilo 28 aliyeshinda timu zingine, huku timu ya Pakaya Ocenic ikimaliza ya pili kwa kumvua samaki mwenye kilo 12.
Nyama choma ilikuwepo katika tamasha hilo la Chakula na Uvuvi.
Mchezo wa uvuvi ushirikisha timu yenye watu kadhaa ambao huenda bahari wakiwa na boti na kuvua samaki kwa kutumia mshipi na ndoano, uvuvi ambao ni salama kabisa kwa samaki hasa ukizingatia kuwa moja ya lengo la tamasha hilo ni kupiga vita uvuvi haramu.

Tamasha hilo lilikamilika kwa burudani kutoka kwa La Rhumba Band pamoja misosi ya nyama choma, ambayo ilipikwa kifundi na wapishi waliobobea kama Mr. Peter na wengine.
Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, Gradys Rutihinda akiwa amelinyanyua juu Kombe la ushindi wa kwanza wa uvuvi.
Rutihinda aliwashukuru watu wote waliofika katika tamasha hilo na kuahidi kufanyika kila mwaka na kuliboresha siku hadi siku na kuvutia watu wengi zaidi huku akitoa wito kwa wadhamini kujitokeza kwa wingi kudhamini tamasha hilo.

Alisema mwaka huu wameliendesh wenyewe kwa gharama zao, ambapo aliwaomba wadhamini kujitokeza ili kumuunga mkono katika harakati zake za kutangaza fursa zilizopo Kilwa na kumuenzi Kipande.


Tamasha hilo lilifanyikia Kilwa Dreams Resort  Kilwa Masoko karibu na pale alipokubwa samaki mkubwa zaidi kuwahi kuonekana mwenye tani 40, urefu wa futi 45 mwnye mbavu kubwa mithili ya mkono wa mtu mzima pamoja na mafuta mengi yanayodaiwa kuponya magonjwa mbalimbali.

Akitanggaza matokeo ya washindi wa uvuvi wa samaki wakati wa tamasha hilo.La Rhumba Band ikikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wakati wa tamasha hilo.
Samaki akipimwa ili kujua uzito wake kamili katika shindano la uvuvi wakati wa tamasha hilo.
Wapenzi wa muziki wakiselebuka wakati La Rhumba ikitumbuiza.

No comments:

Post a Comment