Sunday 23 October 2016

Guardiola ataka manchester City kujadili mzimu wa sare unaoiandama timu yake inayoongoza ligi kwa tofauti ya mabao



LONDON, England
KOCHA wa Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa timu yake sasa inahitaji `kuangalia kwa kina hali iliyopo’ baada ya timu hiyo kutoka sare dhidi ya Southampton ikishuhudiwa timu hiyo ikitoka sare mara ya tano mfululizo bila ya kushinda.

Katika mchezo huo uliochezwa mapema leo Jumapili,  Manchester City imerejea kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu ya England licha ya kuondoka na sare dhidi ya Southampton.

Wageni ndio walikuwa wa kwanza kupata bao ambalo lilipatikana baada ya pasi ya John Stones kumuwezesha Nathan Redmond kumzunuka Claudio Bravo na kufunga bao lililojaa wavuni.

City waliimarika baada ya awali kuzomewa na mashabiki pale walipopata bao la kusawazisha lililofunwa na mchezaji aliyeingia akitokea benchi Kelechi Iheanacho kufuatia krosi fupi ya Leroy Sane.

Kikosi cha kocha Pep Guardiola kilitawala mchezo katika kipindi cha pili lakini kipa wa Watakatifu Fraser Forster ndiye aliyekuwa kikwazo kwa Man City kupata bao.

Man City inaoonoza kwa kuwa na pointi 20 sawa na Arsenal iliyopo katika nafasi ya pili pamoja na Liverpool ya tatu huku City wakiwa juu kutokana na tofauti ya uwiano wa mabao tu.

No comments:

Post a Comment