Thursday, 20 October 2016

Donald Trump aibuka na utata mpya, asisitiza kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu endapo tu yeye atashindaNEW YORK, Marekani
MGOMBEA wa kiti cha Urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Republican Donald Trump (pichani) amesema kwamba yuko tayari kukubali matokeo ya uchauzi huo  “endapo tu atashinda”.

Aliongeza kuwa atakubali "matokeo safi”, lakini atakuwa na haki ya kuhoji matokeo, ambayo atahisi kuwa na figisu figisu

Trump aliyasema hayo wakati wa mkutano wa kampeni huko Delaware, Ohio, ambako alizungumza kwa mara ya kwanza kabisa tangu alipomaliza mdahalo wa tatu na wa mwisho wa wagombea urais uliofanyika alfajiri ya leo Alhamisi.

Mombea huyo alijikuta matatani wakati wa mdahalo huo baada ya kusema kuwa kamwe hatakubali matokeo ya uchaguzi huo.

Wakati muongozaji wa mdahalo huo Chris Wallace alipouliza kama bwana Trump ikiwa atakubali matokeo endapo atashindwa na mpinzani wake mkubwa kutoka Chama cha Democratic Hillary Clinton, Trump alisema atapenda ,atokeo hayo kusubiri”.
 
Meneja wa kampeni wa Trump, Kellyanne Conway, baadae alisisitiza kuwa mombea wake alikuwa na maana kuwa hatakubali hadi pale “matokeo yatakapojulikana wazi”.

Maelezo hayo, yaliibua hasira kutoka kwa baadhi ya wanachama wa  Republicans, ikiwa ni marudio ya maelezo ya Trump aliyedai kuwa uchaguzi huo umejaa mizengwe dhidi yake.

Trump aliwaambia wasikilizaji hao wa Ohio kuwa uchaguzi huo ulikuwa ukizua maswali mengi kuhusu "haki ya nchi hiyo ".

"Kwa kweli napenda kuahidi wapia kura zanu wote na wafuasi wangu na watu wote wa Marekani, kuwa nitakubali matokeo ya uchaguzi huu mkubwa na wa kihistoria bila shaka yoyote-endapo nitashinda,”alisema.

Baadae aliongeza: "Nitakubali matokeo ya uchaguzi safi, lakini pia nitakuwa na haki ya kufunguia kesi ya kuhoji matokeo hayo."

No comments:

Post a Comment