Thursday 16 August 2018

Naibu Spika Awataka Wanafunzi Shule za Filbert Bayi Kusoma kwa Bidii ili Kufaulu Vizuri Masomo



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson akizungumza na wanafunzi wa Shule za Filbert Bayi mjini Zanzibar jana. Wanafunzi wa shule hizo wako kisiwani humo kwa ziara ya mafunzo na michezo.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kupata matokeo mazuri ili kuzintendea haki juhudi wanazofanya wazazi wao kuwasomesha katika shule nzuri zenye huduma bora.

Tulia aliyasema hayo jana mjini hapa wakati alipokutana na wanafunzi wa shule za Filbert Bayi. ambao wamekuja kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za michezo na mafunzo.
Naibu Spika wa Bunge la Muungano, Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na walimu wa Shule za Filbert Bayi mjini Zanzibar juzi.
 Alisema wazazi wanaupendo mkubwa kwa watoto wao na kuhakikisha wanapata elimu bora katika shule nzuri, hivyo wanafunzi hawanabudi kuonesha shukrani kwa kusoma kwa bidii ili kupata matokeo mazuri, kwani hawana sababu ya kushindwa kufaulu.

“Nawatakia kila la heri na sitarajii kabisa mwanafunzi apelekwe katika shule nzuri zenye elimu bora, alafu ashindwe kufanya vizuru, “alisema Tulia huku akiwapongeza walimiliki wa shule hizo kwa kuhakikisha wanafunzi wanapat mahitaji yote muhimu pamoja na elimu bora.

Akizungumza kwa niaba ya shule hizo, Mkurugenzi msaidizi wa shule, Elizabeth Mjema alimshukuru Naibu Spika kwa kukutana na kuwatia moyo wanafunzi hao na kuahidi kufikisha salamu hizo kwa wanafunzi wengine waliobaki shuleni pamoja na viongozi wote wa shule hiyo.


 Zaidi ya wanafunzi 198 wa shule za msingi na sekondari za Filbert Bayi za Kimara na Mkuza Kibaha, wako kisiwani hapa kwa mwaliko wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson akiagana na wanafunzi wa shule za Filbert Bayi baada ya kuzungunza nao jana mjini Zanzibar. Kshoto ni Mkurugenzi msaidizi wa shule hizo, Elizabeth Mjema.
Baada ya ziara ya mafunzo kwa kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria, wanafunzi na walimu wa shule hizo, Jumamosi watashiriki michezo mbalimbali katika Uwanja wa Amaan mjini hapa.

Walimu wa shule za Filbert Bayi wakiangalia hali ya usalama katika pango la watumwa kabla ya wanafunzi wa shuke hiyo hawajaingia katika pango hilo wakati wa ziara ya mafunzo ya shule hiyo kisiwani Zanzibar jana.
Kesho Ijumaa wanafunzi hao wa shule za Filbert Bayi pamoja na walimu wao watatembelea Baraza la Wawkilishi baada ya leo kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria ikiwemo kisima cha chini kwa chini, pango la watumwa, fukwe ambako watumwa walikuwa wakipitishiwa na kupandishwa majahazi baada ya kupigwa bei na kupelekwa Uarabuni, maskani ya Sultani, Stone Town na Forodhani, ambako walipata fursa ya kula urojo.

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Tulia Ackson (kulia) akiagana na Mkurugenzi Msaidizi wa Shule za Filbert Bayi, Elizabeth Mjema mjini Zanzibar jana.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Filbert Bayi wakiingia katika kisima cha chini kwa chini kilichopo Mwangapwani kisiwani Zanzibar leo.
Baadhi ya walimu wa Shule za Filbert Bayi wakiwa ufukwe  wa Bahari ya Hindi leo mjini Zanzibar.
 

No comments:

Post a Comment