Friday 3 August 2018

Mnangagwa Ashinda Kiti cha Urais Zimbabwe

HARARE, Zimbabwe
EMMERSON Mnangagwa (pichani) ameshinda Uchaguzi wa Rais, kwa mujibu wa Kamisheni ya Uchaguzi nchini Zimbabwe, imeelezwa.

Huku majimbo yote 10 yametangaza, Bwana Mnangagwa ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 50.3 dhidi ya mpinzani wake, Nelson Chamisa.

Polisi iliwaondoa viongozi wa wapinzani kutoka katika steji ya Kamisheni ya Uchaguzi wakati wakipiga matokeo.

Mwenyekiti wa Chama cha Bwana Chamisa cha MDC Alliance alisema kuwa kura hizo zilizotangazwa hazikuwa halali.

Rais huyo alishinda kwa asilimia ndogo ya 50 ya kura zote, na kumfanya Mnangangwa amefanikiwa kukwepa kufanyika kwa duru la pili la uchaguzi dhidi ya Chamisa.

Rais huyo alisema kuwa "amefurahi" alisema katika Twitter, na kusema kuwa matokeo hayo ndio mwanzo.

Bwana Chamisa alisisitiza ameshinda uchaguzi huo, aliwaambia waandishi wa habari mapema jana kuwa Chama Tawala cha Zanu-PF kilijaribu kubadili matokeo, kitu ambacho kamwe hawatakikubali.

Lakini Kamisheni ya Uchaguzi ya Zambabwe (Zec) ilisema hakukuwa na udanganyifu yoyote na uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Waandamanaji wa upande wa upinzani walifurika jijini Harare wakipinga matokeo hayo, ambapo watu sita wanadai kufa kutokana na vurugu hizo.

Uchaguzi huo ni wa kwanza kufanyika tangu mtawala wa muda mrefu Robert Mugabe, 94, kutolewa madarakani Novemba mwaka jana.

No comments:

Post a Comment