Wednesday 8 August 2018

RT Yamtakia Kila la Heri Waziri Kigwangalla


Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) limemtakia heri na kupona haraka Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla, ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili akipatiwa matibabu baada ya kuumia vibaya katika ajali ya gari iliyotokea Mkoani Manyara hivi karibuni.

 Katibu Mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday hivi karibuni alitoa tangazo kwa niaba ya shirikisho hilo la riadha, linalomtakia Kigwangalla apone haraka na kurejea katika majukumu yake aliyokabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli.

 Kigwangalla ni mwanamichezo wa ukweli na ni mwanariadha, ambaye hivi karibuni alimaliza mbio za Bagamoyo Historical Marathon zilizofanyika Bagamoyo na kabla ya hapo alimaliza mbio za nusu marathon, yaani kilometa 21 za Ngorongoro Race mjini Karatu na kuwa Waziri wa kwanza kuweza kumaliza mbio za umbali huo.


No comments:

Post a Comment