Sunday 12 August 2018

Mtoto Anusurika Ajali ya Ndege Iliyoua 8 Indonesia

JAKARTA, Indonesia

MTOTO mwenye umri wa miaka 12 amekutwa hai katika mabaki ya ndege iliyoanguka ambayo iliua watu nane nchini Indonesia.

Picha kutoka eneo la tukio la ajali hiyo linamuonyesha mvulana huyo akiwa na fahamu yake huku akiangalia kamera.

Alikutwa katika mabaki ya ndege hiyo katika eneo la milima jirani na mpaka na Papua New Guinea leo asubuhi.

Ndege hiyo iliyotengenezwa Uswisi aina ya Pilatus iliuwa ikisafiri kablaya kupoteza mawasiliano Jumamosi mchana, muda mfupi ikitaka kutua katika Kiwanja cha Ndege cha Oksibil.

Ndege hiyo inamilikiwa na kampuni binafsi ya ndege za kukodi ya Dimonim Air, ilikuwa ikisafiri kutoka Tanah Merah, kama kilometa 40 kusini, kwenda Oksibil katika jimbo la Papua wakati ikitua.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba watu tisa, wakiwemo wafanyakazi wawili.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AFP, vijiji vya jirani vilisikia “muungurumo mkubwa na kufuatia na mlipuko”.

Uchunguzi wa sababu za kuanguka kwa ndege hiyo utatolewa baada ya uchunguzi kukamilika, viongozi walisema.

Ndege ndio njia pekee ya kufika katika jimbo la Papua, sehemu ya ndani na yenye milima mingi ambayo ni ngumu kufika.

Miaka mitatu iliyopita, ndege ya Trigana Air twin ilianguka karibu na Oksibil, na kuuwa watu wote 54 waliokuwemo katika ndege hiyo.

No comments:

Post a Comment