Monday 13 August 2018

Kiboko Amuua Mtalii Aliyetaka Kumpiga Picha


NAIROBI, Kenya

MTALII wa Taiwan amekufa baada ya kushambuliwa na kiboko kifuani wakati akijaribu kumpiga picha mnyama huyo nchini hapa.

Chang Ming Chuang, 66, alikuwa akimtafuta mnyama huyo katika mbuga ya Ziwa Naivasha, kilometa 90 kaskazini-magharibi ya mji mkuu wa nchi hii, Nairobi.

Mtalii mwingine wa pili, naye pia kutoka Taiwan, aliumia. Watu sita wameuawa na kiboko katika eneo hilo mwaka huu.

Maji ya kina kirefu kimeshuhudia vifaru, mnyama hatari anayenyosha na hatari, ametoka katika eneo walikohifadhiwa kutokana na kusaka malisho.

Mamlaka ya Wanyama polisi ya Kenya waliwatambua watalii hao wawili kuwa ni Wachina lakini waziri wa mambo ya nje wa Taiwani baadae alithibitisha kuwa walikuwa ni wataiwani. Kenya haina uhusiano wa moja kwa moja na Taiwani na inakubali madai ya China dhidi ya kisiwa hicho cha Taiwani.

 

Mashuhuda walisema muwa wawili hao waliuwa karibu sana na mnyama huyo jirani na hoteli ya Sopa. Mtu huyo aliyejeruhiwa alikimbizwa hospitalini akitokwa na damu kibao na baadae iliripotiwa kuwa amekufa.

Mtalii mwingine wa pili, aliyejulikana kwa jina la Wu Peng Te, alitibiwa majeraha madogo katika Hospitali ya Wilaya ya Naivasha.

 

Mwenyekiti wa Wamiliki wa Boti katika Ziwa Naivasha, David Kilo alisema kuwa kuongezesha kwa kina cha maji kumepunguza malisho ya viboko, na kuwalazimisha wanyama hao kutafuta malisho katika mashamba na eneo la hoteli, na kuongeza kukaribiana na watu.

 

Viboko, wana meno makali na uzito wao unafikia kilo 2,750 (karibu tani tatu), wanakadiriwa kuua watu 500 kila mwaka barani Afrika.

Utalii unaiingizia Kenya kiasi cha Sh bilioni 1.2bn (sawa na dola za Marekani milioni 950) kwa mwaka.


No comments:

Post a Comment