Thursday 16 August 2018

Paul Pogba Anataka Kuikimbia Manchester United



MANCHESTER, England
PAUL Pogba (pichani) anataka kuondoka Manchester United na kutua Barcelona licha ya kumaliza tofauti zake na kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho.

Man United inasisitiza kuwa mchezaji huyo aliyesajiliwa na klabu hiyo kwa ada,  ambayo ni rekodi ya kiasi cha pauni milioni 89 kamwe hatapigwa bei kwa bei yoyote, lakini Pogba moyo wake ameuelekeza katika kuichezea Barcelona ya Hispania.

Mourinho anajaribu kumshawishi kiungo huyo kuendelea kukipiga katika klabu hiyo kwa kumpatia unahodha katika mchezo wa kwanza wa United wa msimu dhidi ya Leicester. Hatahivyo, uhusiano wao uliingia dosari wakati Pogba aliposema baada ya mchezo huo kuwa hana mpango wa kujadili hali iliyopo sasa bila ya kupigwa faini.

Sportsmail inaelewa kuwa Pogba ana nia ya kucheza soka Barcelona ikiwa ndio sababu kubwa ya Pogba kutaka kuondoka, na kutoelewa na Mourinho sasa imekuwa sababu kubwa.

Inaamini kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, ambaye hajadai ongezeko la malipo, anapenda kuhamia Hispania tangu alipokuwa akitoka Juventus miaka miwili iliyopita.

Hatahivyo, wakala Mino Raiola alishindwa kuvishawishi vigogo vya soka vya Hispania vya Barcelona au Real Madrid, baadae ikaibuka Man United na kuweka rekodi ya dunia kwa ada na kumyankua mchezaji huyo.

Pogba, 25, ambaye awali aliikacha Man United ya Sir Alex Ferguson na kutua Juventus mwaka 2012,alimwambia makamu mwenyekiti mtendaji wa Old Trafford Ed Woodward na wachezaji wenzake kuwa anataka kuondoka tena.

Raiola amekubaliana na Barca maslahi binafsi na mchezaji huyo yenye thamani ya pauni milioni 89.5 katika kipindi cha zaidi ya miaka mitano, lakini United tayari imegomea ofa hiyo kutoka kwa timu hiyo ya Catalans na wanatarajia kuendelea kugomea hadi dirisha la usajili la Hispania litakapofungwa mwishoni mwa mwezi huu.

No comments:

Post a Comment