Sunday 1 October 2017

Tigo Fiesta yatikisa Ali Hassan Mwinyi Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akifungua Tamasha la Tigo Fiesta kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora juzi.

Tamasha la Tigo fiesta limeendelea tena usiku wa kuamkia jumamosi mkoani Tabora.

Akifungua tamasha hilo mkoani humo, mkuu wa mkoa Aggrey Mwanri alisema hii nafasi nyingine kwa mkoa wetu kuletewa fursa kwa wakazi wetu, nawapongeza sana Tigo na Clouds Media. Pia nawasihi vijana kuondokana na mimba za utotoni na utumiaji wa madawa ya kulevya.

 Nandy

Naye meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Gwamaka Mwakilembe amesema, mwaka huu tumeamua kudhamini tamasha hili kubwa kwa lengo la kuwapa burudani wateja wetu na kuendeleza muziki wetu wa ndani, hii itasaidia kuwapatia kipato wasanii wetu na kuendeleza vipaji vyao. Kwa wateja wetu ndani ya msimu huu wataweza kujipatia ofa mbalimbali wanunuapo tiketi kwa tigopesa.


Kwa upande wa burudani yenyewe, jumla ya wasanii 13 walipanda jukwaani kwa nyakati tofauti lakini msanii Ben pol aliingia kivingine alipowashilikisha kikundi cha ngoma za utamaduni wa kinyamwezi cha mapambano na kuimba nao nyimbo tofauti tofauti za kinyamwezi na za Ben ikiwemo wimbo 'Tatu'na kutengeneza 'remix' ya aina yake

Nao kundi la Rostam kama ilivyoada walifunga tamasha kwa kuamsha mashabiki kwa shangwe walipoimba wimbo wao wa 'huku ama kule'.



Wasanii waliopanda jukwaani ni

1.Rostam

2.Ney wa Mitego

3.Darassa

4.Chege

5.Mr Blue

6.Nandy

7.Maua

8.Young Dee

9.Aslay

10.Jux

11.Msami

12.Ben Pol

13.Ommy Dimpoz

Tamasha hilo linaendelea jumapili hii mkoani Kigoma kwenye uwanja wa Tanganyika.






No comments:

Post a Comment