Tuesday 10 October 2017

Messi apiga hat-tric Argentina ikifuzu Kombe la Dunia

QUITO, Ecuador

QUITO, Ecuador

LIONEL Messi amefunga hat-trick wakati Argentina ikitoka nyuma na kushinda ugenini 3-1 dhidi ya Ecuador na kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Russia mwakani.

Brazil wenyewe tayari walishafuzu huku Luis Suarez akizifumania nyavu mara mbili wakati Uruguay ikiichapa Bolivia 4-2 na kufuzu, pamoja na Colombia nayo pia ikifuzu licha ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Peru.

Peru ilimaliza mchakato huo ikiwa katika nafasi ya tano ya Kanda ya Amerika Kusini ya kufuzu kwa Kombe la Dunia na sasa itakutana na New Zealand katika mechi mbili za mchujo zitakazochzwa nyumbani na ugenini.

Lakini Alexis Sanchez na Chile wametupwa nje baad aya kupokea kichapo cha mabao 3-0 ugenini dhidi ya Brazil.

Argentina ilianza siku ikiwa katika nafasi ya sita na kuwa katika hatari ya kuweza kushindwa kufuzu kwa Kombela Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1970.

 

Timu hiyo ilianza vibaya katika mchezo huo uliofanyika katika ukanda wa juu uliopo hapa na wenyeji walikuwa mbele katika sekunde ya 38 kupitia kwa Romario Ibarra likiwa n bao la mapema zaidi kufungwa Argentina katika Kombe la Dunia.

Hatahivyo, Argentina, ambao ni washindi wa pili wa Kombe la Dunia mashindano yalipofanyikia nchini Brazil 2014, walipambana huku Messi akiwa katika kiwango cha hali ya juu.

Messi, ambaye ni bingwa mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa dunia, alisawazisha baada ya dakika 12 baada ya kushirikiana vizuri na kiungo wazamani wa Manchester United Angel di Maria.

Bao lake la pili lilikuja dakika nane baadae kwa shuti kali ndani ya eneo la hatari kabla hajafunga la tatu na kuiwezesha timu yake kufuzu kwa fainali za mwakani za Kombe la Dunia.

MAJAGA KWA CHILE

Chile,ambayo ilitwaa taji la Copa America katika mashindano mawili yaliyopita, ilikuwa nalengo la kufuzu kwa mara ya tatu mfululizo katika Kombe la Dunia baada ya mara ya mwisho kucheza hatua ya 16 bora mwaka 2010 na 2014.

Walianza raundi hiyo ya mwishi wakiwa katika nafasi ya tatu, lakini walishindwa baada yakufungwa mabao mawili na Brazil ndani ya sekunde tatu yaliyofungwa na Paulinho na Gabriel Jesus.

Wakati Peru ikifunga bao la kusawazisha katika dakika za mwisho za mchezo huo dhidi ya Colombia, Chili ilikuwa ikihitaji kufunga tu ili kucheza hatua ya mtoano.

No comments:

Post a Comment