Tuesday 17 October 2017

Wachezaji Munich wakabidhia magari ya anasa

Gari aina ya Uudi, ambayo wachezaji wa Bayern Munich wamekabidhiwa.

MUNICH, Ujerumani

NYOTA wa timu ya soka ya Bayern Munich wamekabidhiwa magari yao mapya ya anasa aina ya Audi AB.

Wachezaji hao kama akina Robert Lewandowksi, Mats Hummels na Javi Martinez wote walipokea `michuma’ yao mipya wakati wacheaji wa kikosi hicho wakisaini autographs wakati wa hafla ya kila mwaka ya kuabidhi magari huko Ingolstadt.

Hatahivyo, wachezaji wengi wa timu hiyo hawakuwepo kwani walikuwa na timu zao za taifa katika mechi mbalimbali za kimataifa.

Audi ni wadhamini wa kuu wa klabu ya Bayern Munich, ambapo imekuwa ikitoa gari kwa kila mchezaji wa timu hiyo tangu mwaka 2002, mwaka ambao walianza kuwa mhisa na vigogo hao wa soka wa Ujerumani.

Sehemu ya mkataba wao ni kuwa kampuni hiyo ya magari kila mwaka itakuwa ikitoa gari kwa kila mchezaji, ambapo wachezaji hao Jumatatu ya wiki iliyopita walikabidhiwa `michuma’ yao.

Karibu wachezaji wa kikosi hicho kila mwaka wamekuwa wakipata mamilioni, walikabidhiwa seti mpya ya matairi, ambapo sio kitu kigeni kwa wachezaji wa mabingwa hao wa Ujerumani.

Lakini gari hizo aina ya Audi zililetwa zikiwa tayari zina majina ya wachezaji hao katika vibao vya namba zikijulikana kama gari rasmi za Bayern.  Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani wanajua kuwa gari hizo zenye namba zinaoanzia na M-DM zitakuwa zikiendeshwa na wachezaji au viongozi wa kikosi hicho chenye maskani yake Allianz Arena.

Herufi  'M' inasimama badala ya 'Munich', wakati ‘'DM' inasimama badala ya 'Deutscher Meister', au Mabingwa wa Ujerumani, kufuatia ubingwa wa Bayern Munich walioupata msimu uliopita.

Wakati Bayern sio mabingwa wa Ujerumani, kitu ambacho hakijatokea kwa miaka ya hivi karibuni- 'DM' inakuwa 'RM', ambayo inasimama kama 'Rekordmeister', au  mabingwa wa kihistoria.

Wachezaji wa Bayern walichukua magari yao huku wakiwa na mashabiki kibao wa timu hiyo waliohudhuria hafla hiyo, ambapo iliwachukua muda kupiga picha na mashabiki hao.

Kikosi hicho kiliungana na kocha mpya Jupp Heynckes, ambaye wiki iliyopita alitangazwa kama mbadala wa Carlo Ancelott.


Kocha huyo atatimiza miaka 72 wakati akiifundisha klabu hiyo kwa mara ya nne, ambapo walishinda taji la Bundesliga mwaka 1989, 1990 na 2013 na lile la Ligi ya Mabingwa mwaka 2013. 

No comments:

Post a Comment