Tuesday 17 October 2017

Kocha Napoli aipa City ubingwa wa Ulaya

MANCHESTER, England

KOCHA wa timu ya Napoli Maurizio Sarri anasema kuwa Manchester City sasa iko viwango sawa kama Barcelona na Real Madrid na inaweza kuendelea kufanya vizuri hadikutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Man City iliyocheza kandanda safi na kushambulia kwa dakika 20 na kufanikiwa jkupata mabao mawili ya kuongoza dhidi ya Napoli katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Etihad juzi lakini Waitalia hao ambao bado hawajapoteza pointi katika Ligi Kuu ya Italia ya Serie A, iling’ang’ania na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Alipoulizwa baada ya mchezo huo kama Man City sasa iko katika kiwango sawa na vigogo vya Hispania na kama inaweza kutwaa taji hilo la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, Sarri alisema: "Ndio, Nafikiri hivyo.

 

"Mana City wana kikosi kisicho cha kawaida. Wako vizuri katika kila idara na wanaweza kufanya vizuri kutokana na ubora wao, “aliongeza kocha huyo.

Kwa ushindi huo Man City inaoongoza katika Kundi F ikiwa na pointi tisa baada ya kucheza mechi tatu na pia inaongoza katika Ligi Kuu ya England baada ya kushinda mara saba kutoka katika mechi nane.

Kikosi cha Guardiola sasa hakijafungwa katika mechi 18 katika mashindano yote, ambapo imeshinda mechi 14 kati ya hizo, tangu walipofungwa 2-1 na Arsenal katika nusu fainali ya Kombe la FA.

Mabao kutoka kwa Raheem Sterling na Gabriel Jesus katika dakika 13 za kwanza yalionekana kufungua mlango kwa Man City kuibuka na ushindi lakini Napoli walijipanga upya na Sarri alisema kuwa amefurahishwa na jinsi walivyojibu.


"Unatakiwa kuugawa mchezo katika dakika 25 za kwanza na baadae zilizobaki. Wanastahili sifa kubwa kwa jinsi walivyoanza mchezo, mbinu za kiufundi, kasi na jinsi movement yao, lakini na sisi hatukuwapa shinikizo kubwa, “alisema.

No comments:

Post a Comment