Thursday 19 October 2017

Multichoice Yatimiza miaka 20 kwa Mbwembwe.. Ofa kabambe kwa watakaohudhuria maonesho Mlimani City!

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Multichoice Tanzania inatimiza miaka 20 toka kuanza kutoa huduma katika soko la Tanzania. 

Multichoice inajivunia mafanikio yake katika soko la Tanzania toka kuanzishwa kwake mwaka 1997, katika kipindi cha miaka 20, tumelihudumia soko la Tanzania Kwa kutoa burudani za kiwango cha juu na ambazo hazipatikani sehemu yeyote ile.

Katika kipindi cha miaka 20 tumewaletea watanzania michuano ya mpira (World Cup, Euro Champions League, Europa League, EPL, La Liga, AFCON na makombe mengine mengi), pia tumeweza kuwaletea maudhui mengi kupitia chaneli yetu ya MNET, Africa Magic na nyingine nyingi.

Multichoice tumekua mstari wa mbele katika kukuza tasnia ya Burudani nchini kwa kipindi chote cha miaka 20 wote mnakumbuka mchango wetu katika mziki kupitia chanel “O” Trace, MTV Base na sasa Trace Mziki. Tasnia ya Filamu tumechangia ukuaji wake kupitia Africa Magic na baadae Maisha Magic East na sasa Maisha Magic Bongo (MMB) ambayo ni maalum kwa kazi za Kitanzania. Tumekuza michezo kupitia uwekezaji wetu kwenye riadha na michezo mingineyo.

Katika Kusheherekea maadhimisho ya miaka 20, Multichoice imeandaa maonesho ya siku 2 yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City kuanzia leo Alhamis Oktoba 19 hadi kesho Ijumaa  kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 11:00 jioni.

 Katika maonesho haya utapata kushuhudia maendeleo ya Teknolojia yetu ya tangu 1997 mpaka sasa na huduma mbali mbali  zitolewazo na Multichoice. Kutakuwa na mabanda kadhaa likiwemo la Supersport, MNET, Maisha Magic Bongo, Fashion, Banda la watoto na mengine mengi.

Kutakua na Ofa kabambe ndani ya siku 2 za Maonesho, ambapo Mteja atajipatia full set ya DStv kwa sh. 59,000 tu  hii ikijumlisha kifurushi cha mwezi mmoja BURE kwa king’amuzi cha HD cha Zappa.

Kwa King’amuzi cha Explora Mteja atapata Kwa sh. 240,000 pamoja na kifurushi cha Compact cha mwezi mmoja BURE…

Ofa hii ni kwa siku za maonesho tu, ambazo ni Alhamisi na Ijumaa hii tu, Hii si ya kukosa!!!


#20YearsOfAwesomeness!!!!!

No comments:

Post a Comment